NEW VIDEO: KALA JEREMAYA FT BEN PO - KARIBU DAR

 

BRAND NEW: LADY JAY DEE FT PROFF JAY - JOTO,HASIRA {official video}

Wakongwe kwenye game ya bongo fleva lady na jd na proff Gzeee waja na project ya pamoja iliyowakutanisha vizuri na kuwafanya mashabiki wao wabaki midomo wazi kutokana na hiyo collabo ambayo haikutegemewa kutoka kwa kipindi hiki ambapo kazi audio imefanyika combination sound chini ya producer man walter a.k.a man maji .
Sasa tayari video imeshatoka na kama bado haujapata nafasi ya kuiona icheck hapo chini
 
 

MISS DAR INDIAN OCEAN YAANZA CHINI YA B HITS



Miss Dar indian ocean imeshaanza na jumamosi ya wikI iliyopita ilikuwa ndIo siku ya audition yake ya kwanza kwa warembo wote waliojitokeza kujaza form za kushiriki kwenye shindano hilo ambalo kwa mwaka hii limeandaliwa na kampuni ya B HITS inayosimamiwa na Harmy B.
Audition ya kwanza ilifanyika katika ukumbi wa much more ambapo walijitokeza washiriki wengi ambao walichujwa mpaka kupatikana warembo 20 ambao wao ndio watakaoanza kambi ya miss dar indian ocan 2013



 
                                                            

Hapa warembo waliojitoketa kwenye audition ya miss dar indian ocean wakisubiri itajwe top 20 ya watakao pita kwenye mchujo wa kwanza.



 
majaji wakiwa na kazi ya kuchaguwa warembo 20 watakaoweza kushiriki miss dar indian ocean
 
baada ya kazi kubwa kufanywa na majaji wa waliokuwa wakiwachuja washiriki wote waliojitokeza hatimae ikapatikana top 20 waliopita kuingia katika shindano la miss dar indian ocean 
 

 
                         top 20 ambao wamepita kuanza kambi ya miss dar indian ocean

 



Baada ya zoezi kukamilika washiriki waliopita wamepewa maelekezao ya nini cha kufanya na waandaji watakutana tena na washiriki hao siku ya jumanne 19/3/2013 saa 11 jion hapo hapo club much more


 


RUNGU LA TCRA LAIKUMBA CLOUDS FM KIPINDI CHAO CHA PIGWA STOP


Makamu Mwenyekiti wa Kamati Maadili ya Utangazaji nchini, Walter Bgoya ( akizungumza na wanahabari leo jijini Dar es Salaam ukumbi wa habari Maelezo.

KAMATI ya Maadili ya Utangazaji nchini imevifungia vituo viwili vya radio pamoja na kukipiga faini kituo cha Clouds FM kutokana na kukiuka maadili ya utangazaji.

Vituo hivyo vya redio ambavyo vyote kwa pamoja vimefungiwa kutorusha matangazo yake kuanzia leo kwa miezi sita ni pamoja na Imani FM cha Dar es Salaam na  Kwa-Neema FM kilichopo mkoani Mwanza.

Akizungumza na waandishi wa habari leo jijini Dar es Salaam, Makamu Mwenyekiti wa Kamati hiyo, Walter Bgoya alisema Kituo cha Clouds FM kimetakiwa kufuta kipindi 
chake cha Jicho la Ng'ombe mara moja pamoja na kulipa faini ya sh. milioni 5.
Akifafanua zaidi Makamu Mwenyekiti huyo alisema vituo vya Imani FM na Kwa-Neema vimefungiwa kwa kosa la kufanya kazi zao kwa uchochezi jambo ambalo ni kinyume cha maadili ya tasnia ya utangazaji. Kituo cha Clouds FM kimetakiwa kutoanzisha kipindi kingine kinacho fanana na Jicho la Ng'ombe.

Kituo cha Imani FM kinadaiwa kufanya uchochezi kwa wananchi juu ya suala la sensa ya watu na makazi huku kile cha Kwa-Neema kufanya uchochezi juu ya mgogoro wa 
uchinjaji wanyama kwa Waislamu na Wakristu mkoani Geita.

Hata hivyo Kamati ya Maadili imeweka mlango wazi kwa vituo hivyo kukata rufaa endapo havikuridhika na adhabu vilivyo pewa kutokana na makosa vinao daiwa 
kufanya.
Kamati Imevitaka vyombo vyote vya habari kufanya kazi kwa kuzingatia Kanuni Sheria na maadili ya tasnia hiyo ili kuepuka kuzua migogoro kwa wananchi ambao wamekuwa 
wakiviamini vituo hivyo.
Hata hivyo mara baada ya ujumbe wa kamati hiyo kumaliza kusoma adhabu hizo kwa waandishi wa habari haukuruhusu maswali kwa waandishi wa habari, hivyo waandishi kubaki wameduwaa


STEVE NYERERE ASEKWA RUMANDE KWA KOSA LA KUSABISHA AJALI SOMA HAPA....



Picha hii inaonyesha Steve akipandishwa gari kuelekea kituo cha polisi.

Ajali hiyo ilitokea  wakati Stive akiwa na baadhi ya washiriki wa movie yake mpya  katika gari lake na wakiwa katika mwendo kuelekea eneo la kushuti sini zao, ghafla aliona gari aina ya funcargo ikiwa imesimama mbele yake huku katikati ya barabara akiwapo jamaa aliyekuwa akisimamisha magari katika eneo hilo.

Baada ya kushindwa kusimama kwa ghafla ndipo alipoigonga gari hiyo kwa nyuma na gari hiyo kutumbukia mtaroni.


Mashuhuda wa ajali hiyo walieleza kuwa chanzo cha ajali hiyo ni Fundi umeme aliyekuwa akisimamisha magari katika eneo hilo ili kuweza kuondoa waya wa Umeme uliokatika na kulala katikati ya barabara huku ukiwa na moto, ili kuepusha madhara zaidi.


Baada ya ajali hiyo, walifika askari Polisi wakiambatana na askari wa usalama barabarani, ambapo alianza kupima ajali hiyo huku madereva wakijibizana na fundi aliyesimamisha magari, ambapo majibizano hayo yaliingiliwa kati na mmoja kati ya askari waliofika eneo hilo.
Katika majibizano hayo baina ya fundi, Askari na madereva wote wawili, ndipo kulitokea kupishana kauli baina ya Steve na Askari huyo, aliyediriki kumuita Stive mjinga, ambapo Steve alishindwa kuvumilia na kuamua kumjibu na ndipo alipokunjwa Shati kaptula na kukokotwa hadi katika gari walilokuja nalo askari hao na kumpakia na kisha kuondoka naye kuelekea katika Kituo cha Mabatini.

Credit:Habari mpasuko 


SAMAKI ALIYEFANANA NA NGURUWE HUYU HAPA

 

HAYA NI MAAJABU..  SAMAKIHUYO AMBAYE ALONEKANA KUWASHANGAZA WENGI KUTOKANA NA MWONEKANO...!!