Napenda kutahadharisha kwamba, picha unayoiona hapo juu haihusiki moja kwa moja na tabia nitakazozitaja kuhusu wanawake wenye sura kama hiyo. Sura hiyo nimeiweka kama kielelezo tu.

Wanawake wenye sura kama hiyo unayoiona ni wanawake ambao kwa kawaida hutamani sana kuwa na maisha ya uadilifu, lakini kuna kuzongwa na saikolojia ya makundi ambayo huweza kuwaharibu sana. Ni wanawake ambao wanapenda sana kufika mbali kimaisha.

Wana tatizo kubwa la kukosa kujiamini au kujiamini kupita kiasi, hasa linapokuja swala la uzuri wa sura au maumbile. Kutokana na hali kama hiyo, wanaweza kuvaa kihasara hasara au kuwa wajeuri bila sababu, ikiwa tu ni njia yao ya kujitetea kutoka katika hisia za kutojitosha.

Ni wanawake ambao wanajua kupenda kwa nje, yaani wakimpenda mtu huonyesha kumjali sana, ingawa kwa ndani sana wanapenda kuona wakilipwa kwa kila wanalofanya kwa wapenzi wao, kwa kifupi ni kwamba wanapenda sana fedha na matanuzi ya hali ya juu. Wanakereka haraka sana, hasa kwenye tendo la ndoa. Wanapenda sana kuona kila wanalotamani wao kwenye suala la tendo la ndoa linakuwa. Kwa hiyo mtu akiwaudhi kwa upande huo, hukereke kupita kiasi.

Kwa kawaida, wana ufahamu wa kutosha na wanapenda kujifunza na kupata mambo mapya. Huwa wanapenda kuonekana kuwa ni watu tofauti kwa kujibainisha kiufahamu. Kama wana kipaji hujitahidi sana kukitumia kwa lengo la kujibainisha kama wao na sio kama wasanii wengine.

Wanaweza kushindwa sana kudumisha ndoa zao kwa sababu ya kutojiamini kwao ambako kwa wapenzi wao huweza kuita ujeuri au ujuaji. Lakini ukweli ni kwamba, siyo wajuaji na wajeuri , bali wanaamini katika kile wanachokiamini. Wana tatizo moja kubwa la kutojali sana kuhusu miili yao, kwa hiyo masuala kama yale ya kushiriki ngono holela ni ya kawaida sana kwao. Siyo ajabu kumkuta mwanamke mwenye sura kama hiyo, akiwa na mabwana kadhaa na kushiriki tendo la ndoa bila kinga wala kujali kitu.

Kuna wakati hutumia miili yao kama chambo, hasa kama wana maumbile mazuri ambayo kwa bahati nzuri kwao, hutokea kuwa nayo. Kama wana makalio makubwa, kwa mfano, hujitahidi yaonekane ili kama mtu anavutika, ababaike au ‘afike bei,’ kama ni lazima. Hata hivyo mara nyingi hutaka tu kuwaumiza watu, kwani hufurahia pale anapopita na watu kuvunja shingo ili kuwaangalia.

Ni wanawake ambao kama wamepata malezi mazuri, huwa na malengo makubwa maishani. Kama wamepata malezi mabaya, huhangaika sana, ingawa bado ile hali ya kuwa na malengo na kutaka kuyafikia huendelea kuwa nayo bado, ingawa siyo kwa kasi kubwa. Ni wanawake ambao wanajua na kuamini kwamba, ni wazuri sana, jambo ambalo wakati mwingine huwafanya kutenda mambo yenye kuwavurugia sifa zao. Kwa kuamini kwao hivyo, hufikia mahali wakajikuta wamezua mitafaruku na kuwafanya wapenzi wao kukerwa nao kirahisi….