JINAMIZI LA VIFO LAHAMIA KWA WAZAZI

Stori: Mwandishi Wetu
inauma sana! Jinamizi lililowaacha watu na majonzi baada ya kufariki kwa mastaa mbalimbali wa hapa Bongo sasa limegeukia upande wa pili na kuhamia kwa wazazi wa mastaa wanaofanya vyema katika kazi zao.

Januari 2, mwaka huu, tasnia ya filamu ilimpoteza msanii mashuhuri, Juma Kiwoloko ‘Sajuki’ na kuwa mwanzo wa vifo vya mastaa wengine.
Kwa mujibu wa utafiti uliofanywa na gazeti hili, Sajuki alipofariki dunia katika Hospitali ya Muhimbili jijini Dar baada ya kuugua kwa muda mrefu, vifo vingine vya mastaa vilifuata kama ifuatavyo:

OMARY OMARY
Gwiji la muziki wa Mchiriku, Omary Omary ambaye alitamba sana na wimbo wa ‘Kupata ni Majaaliwa’ alifariki Juni 8, mwaka huu baada ya kuugua kwa muda mrefu.
Omary alilazwa katika Hospitali ya Temeke jijini Dar na aliruhusiwa siku moja kabla ya kifo chake na aliporudishwa hospitalini hapo akaaga dunia.

MANGWEA
Mfalme wa ‘free style’ mwana Hip Hop, Albert Mangweha ‘Ngwair’ alifariki dunia Mei 28, mwaka huu Afrika Kusini alipoenda kwenye shughuli zake za kisanii.

KASHI
Jinamizi la vifo vya wasanii liliendelea baada ya Juni 10, mwaka huu kumchukua msanii wa filamu, Jaji Khamis ‘Kashi’ aliyefariki dunia katika Hospitali ya Muhimbili.

LANGA KILEO
Safari hii ilikuwa ni kilio tena kwa wasanii wa Hip Hop ambapo  Juni 13, mwaka huu msiba ulihamia kwa Langa Kileo aliyekuwa amelazwa katika Hospitali ya Muhimbili kwa Ugonjwa wa malaria.
JINAMIZI LAHAMIA KWA WAZAZI
Baada ya hapo jinamizi la vifo likahamia kwa wazazi wa mastaa na kuwachukua kwa mfululizo kama ilivyokuwa kwa wasanii.

MAMA DUDE
Msanii wa kwanza kuonja uchungu wa kifo cha mzazi wake mwaka huu ni Kulwa Kikumba ‘Dude’ ambaye alifiwa na mama yake, Mwadodo Ramadhan usiku wa kuamkia Mei 28 wakati akimkimbiza hospitali kwa ajili ya matibabu.

 
MAMA WA Z-ANTO
Kama vile haitoshi, jinamizi hilo lilirudi tena kwa wazazi hao wa mastaa na Julai 11, mwaka huu likamchukua mama wa msanii aliyewahi kutamba na wimbo wa Binti Kiziwi, Ally Mohammed ‘Z- Anto’.
Habari zimesema kwamba mama huyo alifariki dunia kutokana na ugonjwa wa saratani ya ini.

MAMA WA PROFESSA JAY
Siku moja kabla ya kifo cha mama wa Z- Anto, Julai 10, gwiji wa muziki wa Kizazi Kipya, Joseph Haule ‘Profesa Jay’ alipata pigo la kuondokewa na mama yake mzazi, Rosemary Majanjara aliyefariki dunia kwa ajali ya gari maeneo ya Mbezi jijini Dar.


0 comments:

Post a Comment