WENGER AANZA MAZUNGUMZO YA KUONGEZA MKATABA MPYA ARSENAL

 
Kocha wa Arsenal, Arsene Wenger ameanza mazungumzo juu ya kuongeza mkataba wake (HM)
                             
 KOCHA Arsene Wenger yu mbioni kurefusha muda wake wa kuendelea kufanya kazi Arsenal, baada ya kugundulika ameanza mazungumzo ya Mkataba mpya na klabu.
 Mkataba wa sasa wa Mfaransa huyo unaisha majira yajayo ya joto, na ikazua tetesi huenda huo ukawa mwisho wake wa kufanya kazi katika klabu hiyo.
 Lakini Wenger amesema nia yake ni kuongeza Mkataba wa mshahara wa Pauni Milioni 7.5 kwa msimu na mazungumzo ya awali na Mtendaji Mkuu wa klabu, Ivan Gazidis yanaendelea.
 "Kuhusishwa na PSG kupo kwa sababu mimi ni Mfaransa na ninawajua wamiliki. Lakini kama hiyo ndiyo sababu ningekuwa huko tayari.
 "Moyo wangu upo na Arsenal. Mimi si PSG kwa sababu moyo wangu upo na Arsenal,"alisema. 
 Wenger amewasili Indonesia jana kwa ajili ya mechi ya kwanza ya ziara ya Arsenal Mashariki ya Mbali akiwa na mshambuliaji kinda wa miaka 20, Mfaransa Yaya Sanogo, kutoka Auxerre, mchezaji pekee aliyemsajili hadi sasa majira haya ya joto.
 Baada ya miaka kadhaa ya ubakhili, The Gunners itakuwa tayari kubomoa benki sasa kusajili japo mchezaji mmoja wa bei kubwa.
 Wenger anaweza kufanikisha usajili wa Pauni Milioni 23 wa mshambuliaji wa Real Madrid, Gonzalo Higuain, wakati klabu hiyo pia inawataka Wayne Rooney na Luis Suarez.

0 comments:

Post a Comment