MAAFA YA BRAZIL, MAOMBOLEZO YAENDELEA, NI BAADA YA WATU 200 KUFA KWA MOTO

Reuters




Raia wa Brazili wanaomboleza vifo vya watu mia mbili thelathini na watatu waliofariki dunia katika ajali ya moto iliyotokea kwenye ukumbi wa muziki katika mji wa kusini wa Santa Maria.
Maafisa wanasema kuwa wengi wa waathiriwa walikuwa ni wanafunzi waliokufa baada ya kushindwa kupumua kutokana na moshi mkubwa.
Wengine zaidi ya mia moja wanapata matibabu hospitalini . Serikali ya Brazil imetangaza siku tatu za maombolezo . Taarifa zinasema kuwa moto huo ulianza wakati waimbaji wa bendi moja walipowasha fataki.
Maswali sasa yamekuwa yakiulizwa kuhusu usalama wa kumbui za starehe, huku kukiwa na madai kuwa cheti cha huduma za zima moto kilikuwa kimepitwa na wakati. Hili ni jana kubwa la moto kuwahi kuikumba Brazil kwa zaidi ya miongo mitano
Familia za waathiriwa wamekuwa wakiomboleza juu ya majeneza za jamaa zao katika ukumbi wa mamozezi ambao unatuimika kama jumba la kuhifadhia maiti.
Kwa sababu ya heshima kwa waliofariki, serikali iliakhirisha sherehe iliyotarajiwa kufanyika leo Jumatatu katika mji mkuu, Brasilia, kuadhimisha siku 500, kabla ya kombe la dunia kungo'a nagna nchini humo mwaka ujao.
Mazishi ya kwanza mjini Santa Maria yanatarajiwa kufanyika leo , kwa mujibu wa magazeti ya nchi humo.
Maafisa wa utawala wametoa majina ya waathiriwa hao,230 huku maiti watatu wakisalia kutotambuliwa.
Kulingana na taarifa za kituo cha televisheni cha Globo,wengi wa waathiriwa walikuwa kati ya umri wa miaka16 na 20.
Zaidi ya watu 100 wanapokea matibabu baada ya kushindwa kupumua kutokana na moshi mkubwa.

DAWA MPYA YA KUZUIA MAAMBUKIZI YA VIRUSI VYA UKIMWI

                                                         Truvada, dawa mpya ya kuzuia maambukizo ya HIV
Mtu anapogundua kwa mara ya kwanza kwamba ameambukizwa virusi vya HIV hupatwa na mshtuko. Wengine huona kifo kimepiga hodi, wanahofia kumweleza yeyote kutokana na unyanyapaa. 
Lakini leo hii hali imebadilika. Kuna matumaini. Dorothy Onyango ambaye ni muathirika wa HIV kutoka Kenya.Dorothy pia  ni mwenyekiti wa shirika la kina mama wanaoishi na ukimwi nchini Kenya liitwalo WOFAK.
Anaelezea kuwa maendeleo makubwa yamefikiwa kuwapa waathiriwa matumaini na kwamba hivi leo kuna majaribio ya dawa mpya na chanjo. Hizi ni miongoni mwa habari njema kwa waathiriwa na wasio waathiriwa. Anasema ana matumaini kuwa kizazi kisicho na ukimwi chawezekana.
Mama huyo anasema kinyume na ilivyokuwa miaka ya themanini na tisini, waathiriwa wa Ukimwi  sasa wamepata sauti. Wamepata dawa za kudhibiti gonjwa hilo na wanajua namna ya kujitunza na wanaishi  maisha marefu kama watu wengine wowote.
Ni kitu cha kawaida kwa muathiriwa kupatwa na mshtuko mara anapogundua ameambukizwa virusi vya HIV au Ukimwi. Dorothy ambaye ameishi na virusi hivyo kwa zaidi ya miaka 15 anaeleza  kuwa aligunduliwa kuwa na virusi hivyo mapema miaka ya ‘90 wakati huko Kenya mabango makubwa ya watu waliokondeana kwa ukimwi yakiezekwa barabarani na vyombo vya habari kutahadharisha kuhusu gonjwa hilo. Hakumweleza yeyote  kuwa ana virusi vya HIV hadi baada ya miaka mitano.
Nilitaka kujua kimya cha Dorothy cha  miaka mitano baada ya kugunduliwa na HIV aliweza kumudu vipi maisha. Je, alikula chakula cha aina gani au alikuwa na msukumo wa aina gani binafsi kuweza kuishi na kuficha ukweli juu ya hali yake  bila kuonekana kuwa muathiriwa?
Mama huyo anasema alikwenda kimya kimya kwenye mikutano ya waathirwa, na kusoma kila habari zilizoandikwa kuhusu ukiwmi. Alikula vyema na kujitunza. Na huko Kenya dawa ya Kemron iliyotangazwa kuwa inaweza kudhibiti maradhi hayo aliitumia. Alitumia pia dawa nyingine kwa jina Pearl Omega. Lakini baadaye akaamua kuzungumza na wakenya waliokuwa wamejitokeza wazi kueleza  kuwa ni waathiriwa na hivyo kupata msaada wa kimawazo na madawa.
Na kwa wale wanaogunduliwa na HIV na Ukimwi na kutangaza vita vya kusambaza virusi hivyo kwa wengine. Dorothy anawashauri wajilinde wenywe. Anatahadharisha  kuwa wanaweza kudhoofisha afya yao zaidi kwa kupata maambukizo mengine ya zinaa na kukaribisha mauti kabla ya wakati wao.
Anasema mtu akiwa muathirika hakuna njia ya kubadili hali yake kuwa si muathirika, na kwamba kilicho bora kufanya ni kutafuta msaada kuweza kuishi maisha marefu kwa kutumia madwa na kula vizuri. 
Dorothy ambaye amekuwa mwenyekiti wa chama cha wanawake wanaosihi na ukimwi nchini Kenya kinachojulikana kwa kifupi kama WOFAK, anawapa matumaini waathiriwa wa HIV na Ukimwi na anaandika kitabu kuhusu maisha yake na wanawake wengine walioathiriwa lakini wanaoishi maisha ya kawaida.
Na kwa hakika ikiwa wewe ni muathiriwa au una mtu aliyeathirika na virusi vya HIV na Ukimwi fahamu kwamba yapo  matumaini na mifano dunia hii na haswa Afrika ni chungu nzima. Ishi kwa matumaini.
CHANZO; VOA

LOWASA ANUSURIKA




Gari la  Waziri Mkuu Mstaafu na Mbunge wa Monduli na Mwenyekiti wa Kamati ya Mambo ya Nje Ulinzi na Usalama Edward Lowassa likiwa limebonyea kwa ubavuni baada ya kupata ajali iliyotokea jana asubuhi.
Waziri Mkuu Mstaafu na Mbunge wa Monduli na Mwenyekiti wa Kamati ya Mambo ya Nje Ulinzi na Usalama Edward Lowassa Mh. Edward Lowassa amenusurika kifo,baada ya gari lake alilokuwa akisafiria kupata ajali eneo la Bwawani mkoani Morogoro.

Gari hilo la Waziri Mkuu Mstaafu na Mbunge wa Monduli na Mwenyekiti wa Kamati ya Mambo ya Nje Ulinzi na Usalama Edward Lowassa liligongwa na basi la Morobest, wakati basi hilo lilipolipita basi jingine kwenye daraja na kukutana uso kwa uso na gari lakini dereva wa  Mh. Lowasa kwa ustadi mkubwa alilikwepesha gari lisigonge upande alipokuwa amekaa  mzee na kuligonga ubavuni nyuma kwa upande wa dereva na hakuna aliyejeruhiwa.


Waziri Mkuu Mstaafu na Mbunge wa Monduli na Mwenyekiti wa Kamati ya Mambo ya Nje Ulinzi na Usalama Edward Lowassa na msafara wake aliendelea na safari hadi morogoro ambako ameshiriki katika harambee ya ujenzi wa kanisa la KKKT Kilakala ambapo yeye na Marafiki Zake Wamechangia Shilingi Milioni 18

WABUNGE WALIOCHOMEWA NYUMBA WAANGUA KILIO



WABUNGE waliochomewa nyumba na mali zao katika vurugu zilizotokea Mtwara juzi; Anna Abdallah na Mariam Kasembe, jana waliangulia vilio walipotakiwa na mwananchi  kuzungumzia tukio hilo.

Nyumba za wabunge hao wa Viti Maalumu na mali zingine kadhaa za taasisi mbalimbali, ni miongoni mwa vitu vilivyoharibiwa katika vurugu hizo ambazo pia zilisababisha vifo vya watu wanne wilayani Masasi.

Akizungumza kwa huzuni,  Anna alisema hajui sababu za uharibifu huo, hasa ikizingatiwa mwenyewe amekuwa huko kwa karibu siku tatu na hakuona dalili za uhasama wowote dhidi yake.

Anna ambaye pia ni Mwenyekiti wa Bodi ya Korosho alisema: “Nina siku ya tatu hapa Masasi na nimeshiriki mkutano wa halmashauri kwa mwaliko na wakati wote, sikuhisi chochote hivyo siwezi kujua sababu ya chuki iliyofanya nyumba yangu ichomwe moto,” alisema.

Alipotakiwa aeleze hali ilivyokuwa, alisema, “Wavamizi hao walipora kila kitu nyumbani kwangu yakiwamo mapazia, kabla ya kumwaga petroli kila chumba na kuwasha moto.”

Aliendelea kueleza,” Kila kitu kiliteketea. Inatia uchungu kwani nyumba hiyo niliijenga kwa kudunduliza fedha kidogo kidogo nikiwa mkuu wa mkoa.”

Anna alisema, kundi hilo la vijana lilivamia nyumbani kwake saa 4:00 asubuhi na kuanza kupora mali kwa kupita chumba kimoja baada ya kingine.

“Hali si nzuri. Kila kitu kimeibwa na nyumba imechomwa moto, hakuna kilichobaki. Walichukua kila kitu na itanichukua muda mwingi kujua thamani halisi ya hasara iliyopatikana,” alisema.

Kauli ya Kasembe
Naye Kasembe alipokea simu ya mwandishi wa habari hii kwa kilio na kuikata huku akisema, “Jamani niacheni… Mwenzenu naumia…!”


Alipopigiwa tena baadaye, alisema anashangazwa na tukio hilo ambalo limemfika bila kutarajia na kumtia hasara kubwa.

“Wamepora kila kitu katika nyumba na kuichoma moto, sijui atakuwa nani huyu, kwani sina tatizo na wapiga kura wangu na sina mgogoro na mtu yeyote. Nashindwa hata kuhisi nani kafanya uchochezi,” alisema Kasembe.

Alisema wakati wa vurugu hizo, ndugu zake akiwamo mama yake, walikimbia na kwenda kujihifadhi hotelini, lakini mpaka sasa hawajui wataishi vipi baada ya nyumba hiyo kuteketezwa kwa moto.

“Jana wanafamilia walilala hotelini na leo tupo nje ya gofu la nyumba yangu ambayo imeteketea kabisa kwa moto, tunasubiri majaaliwa mengine, lakini nimechanganyikiwa kwa kweli na sijui ni kitu gani hiki, siamini,”alisema.

Polisi waeleza uharibifu
Watu 44 wanashikiliwa na polisi wilayani Masasi kufuatia vurugu hizo.


Kamanda wa Polisi Mkoa  wa Mtwara, Maria Mzuki alisema watu hao wamekamatwa kwa wakituhumiwa kujihusisha na vurugu hizo zilizosababisha uhalibifu mkubwa mali.

0 comments:

Post a Comment