CPWAA AJIPANGA KUKUZA VIPAJI VIPYA


wa miondoko ya muziki wa kizazi kipya Ilunga Khalifa Cpwaa anajipanga kwa ajili ya kuanzisha 'Academic' ili kukuza vipaji vya 'madensa' ambao wanaonekana kufanya kazi kubwa ya kupendezesha shoo za wanamuziki wa bongofleva

Aliyasema hayo jijini Dar es Salaam alipokuwa anaeleza mikakati ya kuibua vipaji vya madensa na jinsi ya kuviendeleza huku akiamini kuwa atakuwa ametoa mchango mkubwa wa kutoa ajira kwa vijana

Alisema kuwa kuanzisha kwa kundi hilo ni moja ya kutoa fursa kwa vijana ambao wenye uwezo na wamekosa nafasi ya kuonyesha vipaji vyao, na kujikwamua kimaisha kupitia vipaji hivyo

"Nampango wa kuanzisha darasa kwa ajili ya wacheza shoo tu itakuwa na mfanano wa kundi la THT kwani nia yangu ni kuwapa heshima na kuthamini mchango wa madensa ambao sasa wanatumika sana na wanamuziki wa bongo fleva" alisema Cpwaa

Pamoja na hayo aliongezea kuwa ili kuonyesha ana nia ya dhati ameanza na kundi la 'Choclate' ambao mpaka sasa wanafanya vizuri na wameweza kuibuka washindi katika mashindano mbalimbali ya 'danse'

Mbali na hayo Cpwaa alisema kuwa anakaribia kuachia video ya nyimbo yake mpya inayojulikana kwa jina la 'Mambo' ambapo sasa yupo katika hatua za mwisho kukamilisha video hiyo

0 comments:

Post a Comment