STEVE NYERERE ASEKWA RUMANDE KWA KOSA LA KUSABISHA AJALI SOMA HAPA....



Picha hii inaonyesha Steve akipandishwa gari kuelekea kituo cha polisi.

Ajali hiyo ilitokea  wakati Stive akiwa na baadhi ya washiriki wa movie yake mpya  katika gari lake na wakiwa katika mwendo kuelekea eneo la kushuti sini zao, ghafla aliona gari aina ya funcargo ikiwa imesimama mbele yake huku katikati ya barabara akiwapo jamaa aliyekuwa akisimamisha magari katika eneo hilo.

Baada ya kushindwa kusimama kwa ghafla ndipo alipoigonga gari hiyo kwa nyuma na gari hiyo kutumbukia mtaroni.


Mashuhuda wa ajali hiyo walieleza kuwa chanzo cha ajali hiyo ni Fundi umeme aliyekuwa akisimamisha magari katika eneo hilo ili kuweza kuondoa waya wa Umeme uliokatika na kulala katikati ya barabara huku ukiwa na moto, ili kuepusha madhara zaidi.


Baada ya ajali hiyo, walifika askari Polisi wakiambatana na askari wa usalama barabarani, ambapo alianza kupima ajali hiyo huku madereva wakijibizana na fundi aliyesimamisha magari, ambapo majibizano hayo yaliingiliwa kati na mmoja kati ya askari waliofika eneo hilo.
Katika majibizano hayo baina ya fundi, Askari na madereva wote wawili, ndipo kulitokea kupishana kauli baina ya Steve na Askari huyo, aliyediriki kumuita Stive mjinga, ambapo Steve alishindwa kuvumilia na kuamua kumjibu na ndipo alipokunjwa Shati kaptula na kukokotwa hadi katika gari walilokuja nalo askari hao na kumpakia na kisha kuondoka naye kuelekea katika Kituo cha Mabatini.

Credit:Habari mpasuko 

0 comments:

Post a Comment