Kahaba anusurika kifo. Apigwa kikatili na wenzie wakidai “anauza” bei rahisi na kuwaharibia soko

Kahabaz



Kahaba mmoja katika mji wa Naivasha, jimboni Rift Valley, Kenya alinusurika kufa baada ya kupewa kichapo cha mwizi na makahaba wenzake kwa sababu wamekerwa na kitendo chake cha kuuza ngono kwa bei rahisi na kuwaharibia soko. Wenzake hao wenye hasira walimtwanga kwa mangumi na mateke, wakimshutumu kwa kutokuwa na ushirikiano na “kuharibu soko” hasa ukizingatia ilikua ni kipindi cha mwisho wa mwezi, ambapo wateja wamejaa mkwanja na mahitaji ya kununua ngono yameongezeka.
Wakati wakimpa kichapo, walitaka kumkeketa (kumtahiri mwanamke) kwa kutumia chupa iliyovunjika “ili iwe funzo” lakini akaokolewa na walinzi wa usiku (wengi wao ni wateja wake) kabla hajafanyiwa kitendo hicho.
Msuguano ulianza mwezi uliopita pale msichana huyo mwenye umbo nyororo na la kuvutia alihamia mitaa hiyo kitu ambacho kiliwakera makahaba wazoefu hapo maana walimuona kama tishio kutokana na urembo wake.
Kwa mujibu wa dereva wa bodaboda anayeitwa Peter, kahaba huyo amekua ni kivutio na anayependwa na wengi kutokana na uzuri wa umbo lake na rangi nyeupe ya ngozi yake. Zaidi ya “kupunguza bei,” inadaiwa kuwa kahaba huyo pia anatoa “huduma” kwa mkopo, kitu ambacho wenzie hawafanyi, hivyo kuzidi kuwaaribia biashara zaidi.
“Kwa kawaida, bei ni kati ya Ksh 100 mpaka Ksh 500 (kama TZ Shs 2,000 mpaka 10,000) inategemeana na mteja. Lakini “Brownie” anauza kwa hata Kshs 50 (TShs 1,000)” alidai Peter.
Idadi ya wateja wake ilikua kwa wingi na kwa kasi, kitu kilichopelekea wivu na chuki kutoka kwa makahaba wengine, ndipo walipofikia uamuzi wa kufanya njama za kupanga kumpa kichapo “ili iwe fundisho.”
Makahaba hao walitekeleza lengo hilo pale walipomzingira kwenye kona, gizani akiwa peke yake, na kumshambulia kikatili.
“Kwani unafikiria sisi tutakula wapi kama utaendelea kujiuza hii bei hasara.” Mmoja wa wanawake hao alimkaripia kwa sauti ya juu.
Kahaba huyo alipiga mayowe na kuomba msamaha kutoka kwa wanawake hao wenye hasira wakati anashambuliwa, ndipo walinzi waliposikia na kukimbilia kumuokoa.
Walinzi hao walipofika, walikaripiwa na makahaba hao wakiambiwa kuwa hiyo ni ishu ya wanawake, na wao haiwahusu.
““Unajua huyu mama huwa ananipatia kwa mkopo siku ninazokuwa nimechacha hivyo siwezi muacha auliwe na hawa mikora” alisema mmoja wa walinzi hao wakati wakijaribu kumuokoa mwanamke huyo.
“Wateja” wake wengine wakaingilia kumuokoa kahaba huyo ambaye alikua ameumizwa vibaya, na kumkimbiza hospitali.
Inaonekana makahaba wazoefu maeneo hayo wanatawala “ngome” yao na lazima wakatiwe panga na makahaba wapya, ambao lazima wajitambulishe kabla ya kujiunga kwenye “soko” lao.
“Brownie” bado yuko hospitali akipatiwa matibabu huku wateja wake wakimsubiri apone, ili waendelee kupata “huduma” zake kwa bei nafuu, na kwa mkopo.
“Maisha imekuwa ngumu sana na bei ya kila kitu, hata ya hawa wasichana imepanda sana. Tunaomba serikali iingilie kati ,” mmoja wa walinzi hao alilalamika.

1 comments:

  1. Casino Slots Review - JTM Hub
    Casino 여주 출장샵 Slots Review: ✓ The Best Casino Slots Games ✓ Best Mobile Casino Games ✓ The Best Welcome Bonus ✓ Mobile Casino 파주 출장샵 Games Bonus: 100% up 전라남도 출장안마 to $/€ 전주 출장마사지 50 김제 출장안마

    ReplyDelete