Kero za watoa huduma kwa wateja


Unapokuwa mtoa huduma kwa wateja (customer care) unatakiwa kuwa sharp, kauli nzuri na tabasamu kwa watu unaaowahudumia.

Hii imekuwa tofauti kwa watoa huduma wengi hapa Tanzania sijajua huko sehemu nyingine. Unafika sehemu unapokelewa na uso umekunjwa na majibu ya nyodo hasa ukiwa mrembo na mtoa huduma ni mwanamke! Wengine watu wanasubiri huduma mf; benki yeye anaongea na simu kwa mapozi yaani hana habari wala hajali ile foleni mliyopanga kumngoja yeye.


Wakati mwingine unaulizia huduma unahitaji maelezo ya kueleweka ila jibu utalopewa unaweza kukaa chini ulie! wanajisahau kama ile ni kazi inayomlipa mshahara na anatakiwa aitumikie.

Tubadilike jamani kama unahusika kutoa huduma kwa wateja unatakiwa uwe mkarimu,hujui unaye mfanyia nyodo ni nani au mnaweza kukutana wapi siku za usoni na wewe ukahitaji msaada wake maana unaweza kumjibu hovyo mkweo.Tunaishi kwa kutegemeana kama binadamu kwa hiyo kukaa mapokezi au kuwa customer care kusikuvimbishe kichwa ukajiona umefika.

Maboss nao wanatakiwa wawe makini na watu wanaowaajiri kwa ajili ya huduma hizo. Pia uanpoletewa malalamiko na wateja ili kulinda heshima ya ofisi yako unatakiwa uyazingatie na kuyafanyia kazi.Kwa leo naishia hapa inaowahusu ujumbe wamepata.

0 comments:

Post a Comment