Aibiwa Laptop kwenye foleni barabara ya Nyerere

MKAZI wa jijini Dar es Salaam [mwanaume] jina lake halikuweza kupatikana mara moja, amejikuta akishindwa kuendesha gari, baada ya kuporwa kompyuta aina ya Laptop akiwa kwenye foleni katika barabara ya Nyerere
Tukio hilo lililoshuhudiwa na mwandishi wa habari hii jana majira ya jioni, dereva huyo alijikuta akisababisha foleni baada ya taa kuruhusu na yeye akijikuta akiduwaa mara baada ya kumtokea tukio hilo

Mkazi huyo wa jiji alikuwa akiendesha gari ndogo aina ya Toyota huu mapajani mwake akiwa ameweka Laptop hiyo kwa matumizi yake pindi alipokuta foleni

Kwa kawaida majira ya jioni katika barabara nyingi jijini hususani hiyo ya Nyerere hukabiliwa na foleni inayofanya kupatikana kwa kero kwa watumiaji wake

Hivyo kutokana na foleni hiyo ambayo yeye aliiona anaweza kufanya mambo yake mengine, akaamua kutumia komputa yake hiyo akiwa kwenye foleni hiyo bila kutambua kuna wezi wanaotalii kuangalia huko na kuko kwa anayezubaa ajinyakulie mali aina yoyote kwa abiria wanaotumia daladala ama waliokuwa kwenye usafiri binafsi kisha kukimbia

Ghafla foleni ilipokaribia kwenda akatokea kibaka mmoja kusogelea kwenye gari hilo akamnyang’anya komputa hiyo na mmiliki huyo kubaki akiduwaa na alipochukua uamuzi wa kumkimbiza hakuona hata vumbi lake

Huku baadhi ya watu walioona tukio hilo waliokuwa kwenye foleni walimshauri arudi garini kwa kuwa asingemuona tena mwizi wake huyo

Hivyo muda wa kuruhusu magari kwa upande unaotokea mjini kuelekea maeneo ya Uwanja wa Ndege ukawadia kutakiwa magari yapite kwenye foleni dereva huyo alijikuta akisababisha foleni kwa kuduwaa licha ya madereva wenzake kumuamuru aondoe gari hilo

Hata hivyo honi hazikuweza kuzaa matunda hadi pale baadhi ya madereva walioshuka kumuamuru asonge mbele kwa kuwa tayari foleni ilisharuhusiwa ndipo aliposonga mbele

0 comments:

Post a Comment