MTOTO WA MIAKA 6 ANONYESHA KIPAJI CHAKE CHA KUIGIZA





Mtoto mwenye umri wa miaka 6 anayeishi kinondoni jijini dar amejitokeza jana kwenye mkutano wa shirikisho la filamu Tanzania uliokuwa ukifanyika vijana pale kinondoni ili akutane na wasanii wakubwa apate nafasi ya kuzungumza nao na kuonyesha uwezo wake na kipaji alichojaliwa katika kuigiza.

 mtoto huyo aliyejulikana kwa jina moja tu la oliver mwenye miaka 6 aliletwa kwenye mkutano huo na dada yake anajulikana kwa jina la shakira ambae pia ana mapenzi na fani ya uigizaji kupitia bongo movie.

 kwa bahati mbaya oliver  hakupata nafasi ya kuongea na msanii yoyote mkubwa ambae alikuwepo hapo kwenye kikao ambae yuko kwenye game ili aweze kumsikiliza na kumsaidia



chokoza ilipata nafasi ya kuongea na dada aliyeongozana na mtoto huyo OLIVER kujua zaid juu ya kipaji chake.
NUKUU " Tumegundua kipaji chake baada ya kumkuta mara nyingi akiwa anaongea peke yake na wakati mwingine akiwa chumbani anaigiza matukio mbalimbali ambayo yanahashiria kuwa anatamani kuja kuwa muigizaji mkubwa ndo maana tuka chukua uamuzi wa kumlete hapa ambapo wamekusanyika wasanii wengi wakubwa wa bongo movie"

 kutokana na kukosa nafasi ya kuongea na msanii yoyote kati ya wote waliokuwapo kesho pia mtoto oliver atafanikiwa tena kufika pale vijana ambapo kutakuwa na mkutanoo wa shirikisho la filamu na waandishi wa habari.




kama we ni msanii na unaweza kusaidia maendeleo ya mtoto huyu katika kuendeleza kipaji chake unaweza kuwasiliana nae kwa simu no 0718648624 au 0655232320


0 comments:

Post a Comment