Picha ya Rais Kikwete alipomtembelea hospitali tajiri aliemwagiwa tindikali


Msasani City Mall
Msasani City Mall ambalo Said anatajwa kuwa mmiliki wake.
Mmiliki wa Homeshoping centre na Msasani City mall kalazwa South Afrika July 26 2013 JK Kamtembelea

Said anatajwa kuwa mmiliki wa maduka ya Home shopping centre na pia mmiliki wa jengo jipya ambalo limechukua headlines Dar es salaam la Msasani City Mall ambalo ndani yake kuna maduka ya nguo na viatu.. yote yakiwa yanamilikiwa na yeye tu.
Siku kadhaa zilizopita alimwagiwa tindikali na mtu ambae hakufahamika ambapo muda mfupi baadae alikimbizwa hospitali Afrika Kusini kwa ajili ya matibabu ambapo Rais Jakaya Kikwete mtu wa watu ni miongoni mwa waliokwenda kumjulia hali kama unavyomuona kwenye picha.
Moja kati ya Magazeti pendwa wiki hii yalitoa ripoti kwamba Said ndio anatajwa kuwa tajiri kuliko wafanyabiashara wote Kariakoo Dar es salaam.
Msasani City Mall kwenye moja kati ya maduka yake ndani
Msasani City Mall kwenye moja kati ya maduka yake ndani

0 comments:

Post a Comment