MATOKEO YA KIDATO CHA NNE MWAKA 2012 KUTANGAZWA HIVI KARIBUNI HUKU KUKIWA HOFU KUBWA KWA WANAFUNZI HAWO:
WASIWASI mkubwa umeigubika jamii katika kipindi hichi kigumu kwa wanafunzi wa kidato cha nne kusubiri matokeo kutangazwa kutokana na haki halisi ya migomo ya walimu iliyolikumba taifa kwa mwaka jana (2012). Hali hiyo inatokana na hali ilivyokuwa kwa watahiniwa wa kidato cha pili ambapo matokeo hayakuwa mazuri kwa mwaka huu, na pia hali imedhihirika katika mitandao ya kijamii kama facebook, whatsup na twitter.
RAY AFUNGUKA NA KUSEMA SIMUOI MAINDA WALA JOHARI, WATANIUA KWA PRESHA
Stori: Imelda Mtema KATIKA kile kilichotafsiriwa kuwa ni kuwafutilia mbali wasanii wenzake, Blandina Chagula na Ruth Suka ‘Mainda’ aliowahi kudaiwa kutoka nao kimapenzi, staa wa filamu Bongo, Vincent Kigosi amefunguka kuwa, hatarajii kuoa msanii kwani anaogopa presha. |
Vincent Kigosi.
Akizungumza na Ijumaa hivi karibuni, Ray alisema kuwa anajua matatizo ya kuoa staa hivyo ili kuepukana nayo ameamua kuwekeza penzi lake kwa mwanamke anayefanya kazi benki (jina amelihifadhi kwa sasa) akidai kuwa huyo ndiye tulizo la moyo wake.
Ruth Suka ‘Mainda’.
“Kaa ukijua kuwa sina mpango wa kumuoa staa yeyote, mwanamke ninayetarajia kumuoa ni mfanyakazi wa benki na mipango yangu ikikamilika nitakueleza kila kitu. Mimi sitaki presha bwana,” alisema Ray.
Blandina Chagula 'Johari'.
WEMA AIONYESHA PICHA YA LIFATAKI LAKE KUPTIA MTANDAO
Wema Sepetu akiwa kimahaba na mwanaume aliyedai ni 'mumewe'.
Picha hiyo ambayo aliiweka kwenye mtandao wa BBM inamuonesha msanii huyo akibusiana na mwanaume huyo lakini wakionekana kuanzia kwenye kidevu hadi kwenye kiuno.Baada ya kuitupia picha hiyo, Wema aliandika: ‘Miss you mume wangu, wewe ndio kila kitu katika maisha yangu, watasema sana lakini mambo yetu yanatuendea vizuri.” Maneno hayo yanaashiria kuwa Wema anampenda sana mwanaume huyo ambaye siyo Diamond. |
0 comments:
Post a Comment