WAMA YASAIDIA HOSPITALI YA MKOA WA LINDI VIFAA TIBA




Wama yakabidhi vifaa kwa Hospital ya mkoa wa Lindi
Taasisi ya Wanawake na Maendeleo(WAMA)Katika kusaidia sehemu kubwa ya
Jamii na  makundi yenye kuhitaji msaada hususan Wanawake,watoto na
wasio na uwezo ufadhili wa Taasisi mbalimbali Nchi Za Nje ili
Kuboresha Huduma za Afya hapa Nchini Imetoa msaada wa Vifaa tiba kwa
Hospital ya Mkoa wa Lindi
Hayo yamebainika katika Hafla fupi ya kukabidhi Vifaa tiba kwa Vyenye
thamani ya Milioni 700 vilivyotolewa na Shirika la Project Cure la
Marekani baada ya Taasisi hiyo kuchangia na leo kukabidhiwa kwa Vifaa
hivyo kwa  Mkoa huo na Mwenyekiti wa Taasisi hiyo ambae Pia ni Mke wa
Rais,Mama Salma Kikwete kueleza kuwa licha kukabidhi msaada huo
misaada zaidi ya WAMA ipo katika nyanja za elimu, afya pamoja na
maendeleo ya wanawake katika mikoa yote Nchini.
Aidha alibainisha kuwa pamoja na taasisi ya WAMA kupata mafanikio
katika kupunguza idadi ya vifo vya mama na mtoto, mapambano dhidi ya
Malaria na UKIMWI, chanjo kwa watoto ikiwemo ya ugonjwa wa Nimonia,
mimba kwa wanafunzi wa kike pamoja na kuwawezesha wajasiriamali wa
kike hapa nchini Pia ametoa wito kwa Wakazi wa Lindi kusimamia Elimu
ya Watoto.
Kwa upande wake Mwakilishi wa Shirika la Project Cure la Marekani.Bw
Abdu Kimario ameipongeza taasisi ya WAMA kwa mchango wake katika jamii
hasa kuboresha elimu, huduma za afya pamoja na mapambano dhidi ya
mimba za udogoni kwa wanafunzi wa kike na kuwaendeleza wajasiriamali
wa kike nchini na kubainisha kuwa Vifaa kama hivyo vilivyokabidhiwa
leo pia vitakabidhiwa katika mikoa mingine Nchini Hivi Karibuni
Kwa upande wake Kaimu Mganga Mkuu wa Mkoa wa Lindi,Dr Richard Boniface
alieleza jinsi msaada huo utakavyosaidia kufuatia kutowepo kwa huduma
ya X-ray kwa zaidi ya mwaka mmoja hata hivyo pamoja na msaada huo pia
aliomba ufadhili zaidi wa Elimu kwa watumiaji wa Vifaa tiba hivyo
Vifaa vilivyokabidhiwa leo ni pamoja na Mashine ya X-ray pamoja na
vifaa vyake vyote,Mitambo ya kitanda maalum cha ICU Kwa ajili ya
wagonjwa mahututi,Mitungi ya gesi ya Oxygen ambayo itasaidia kutoa
huduma ya dharura hasa wakati Umeme umekatika,Vifaa na mitambo kwa
ajili ya huduma za kinywa na meno,Vifaa vya upasuaji mdogo na
mkubwa,Ultra sound machine,Taa,meza na mashine ya Usingizi

0 comments:

Post a Comment