KIFAA KIPYA KUTOKA KAMPUNI YA GOOGLE
Mwanzoni mwa mwaka huu, Google iliniuliza kama
nitapenda kujaribu kutengeneza programu ambayo itakua inahusiana na matumizi
mbalimbali ya google glass, kwakuwa hua napenda kujaribu kufanya kazi
mbalimbali nilisoma maelezo niliyopewa na Google na nilivutiwa sana.
Matumizi ya programu na tecknolojia ya Google
glass imekua ni ndoto ya muda mrefu ya watumiaji wa tecknolojia mpya ambao
wamekua wakiutazama ulimwengu kama sehemu ambayo mawasiliano yanakua karibu nao
sana.
Google Glass inaweza kutupa ukweli wa ndoto ya mda mrefu ambayo wengi
wamekuwa wakiihitaji, lakini kwa kutekeleza hilo kunaibuka maswali mengine
mapya, je bado tutakua tunahitaji zaidi ya hapo wakati tayari tunaitumia google
glass? Je itafanya maisha kua magumu au itayarahisisha? Na je maelekezo yake ya
usiri (privacy) ya mtu yatakua yanajali utamaduni?
Mdahalo ndo kwanza umeanza, kwa upande wangu nafikiri tatizo
kubwa la mifano mingi ya tecknolojia kama google glass ni kwamba msisitizo
unawekwa sana kwenye tecknolojia yenyewe kuliko kwenye namna halisi ya uvaaji
au utumiaji wake. Ili kuongeza maombi ya idadi ya watumiaji wakati Google glass
ikiingia rasmi sokoni, Google itazingatia kwa makini njia ya kuunda mfumo mzuri
ili kuepuka kuonekana kama kikwazo.
Itakua vizuri kuweka mahusiano mazuri na wabunifu mbalimbali wa miwani
(glass) kama Tom Ford au Ray-Ban ili kutengeneza kitu ambacho kitaridhisha watu
na watamani kuvaa. Nilikosa amani nilivyokua natakiwa kutoa maelekezo kwa
ishara , hili pia ni tatizo langu na Siri pamoja na tecknolojia nyingine
zinazotumia sauti kutoa maelekezo (voice-activated technology), nani anataka
kuwa mjinga kuongea peke yake na kompyuta. Kwa saivi nilipendekeza kwa
wawakilishi wa Google kwamba labda wanaweza kuwa na mawani yanayoweza kutambua
aina Fulani ya lugha ya ishara na badae mtu anaweza akavaa pete au bangili
yenye kifaa kidogo ambacho kina uwezo wa kusoma matendo yako na kuyawasilisha
kwa mawani.
Miezi michache ijayo baada ya kuingia sokoni Google Glass itakua na
ushindani wa ghafla na tecknolojia nyingine zenye matumizi ya tecknolojia ya
mawani kutoka kwa Apple na Samsung. Apple inatumia inchi 1.5 OLED screens
ambazo zinafaa kwa “iwatch” , Samsung imethibitisha maendeleo ya smartwatch, na
inasemekana kwamba mbinu ya smartwatch itakua rahisi na inayokubalika zaidi
kutumia japokua haina huduma kubwa ya mawasiliano kama tecknolojia nyingine.Karne ya tecknolojia ya kuvaa mawani ambayo google glass na smartwatches inatupeleka itakua kama soko la technolojia ya smartphone miaka saba iliyopita. Utaratibu mmoja naouona unatawala tecknolojia hii mpya ni kwamba ili tecknolojia ya mawani ilete maana inatakiwa kuyaboresha maisha yetu ipasavyo na sio kuyafanya yawe magumu au kuyaingilia bila mpangilio.
0 comments:
Post a Comment