LAANA: BABA ANASWA AKIMBAKA KUKU HADHARANI.
MWANAMUME mmoja huko Kenya katika kijiji cha Kigwandi, wilayani Tetu
anazuiliwa katika kituo kimoja cha polisi mjini Nyeri baada ya
kufumaniwa akifanya tendo la ngono na kuku.
Mwanamume huyo mwenye umri wa zaidi ya miaka 50 alikamatwa Alhamisi jioni.Kaimu
afisa mkuu wa polisi katika eneo hilo, Bw Joseph Mwika alisema mwanawe
mwanamume huyo mwenye umri wa miaka 10 alimuarifu ka'kake mkubwa baada
ya kumfumania babake akifanya kitendo hicho na ndipo wawili hao
walimripoti baba yao kwa chifu wa eneo hilo ambaye alimkamata na
kumpeleka katika kituo cha polisi.
“Kuku
huyo alikuwa wa mwanawe mwanamume huyo aliyeripoti kisa hicho kwa
chifu... Kuku huyo ambaye baadaye alikufa alipelekwa katika maabara ili
kufanyiwa uchunguzi. Tunasubiri matokeo ya madaktari wa mifugo kabla ya
kuchukua hatua,” alisema Bw Mwika
0 comments:
Post a Comment