
AMESEMA…… ‘mi mwenyewe nimezisikia hizo habari na zimenishtua lakini katika kuja kufatilia nikagundua kwamba majina yamegongana, kuna mtu mwingine anaitwa Linah ambae amepatwa na hilo jambo, sikutoka nyumbani kwa siku tatu… yani nilikwenda tu movie na kurudi nyumbani, katika kufatilia nilimnukuu mtu alieniambia kwamba rapper Kalapina alikua ameziandika facebook ila sio Linah mimi, usumbufu nimepata mkubwa sana mpaka nyumbani wamenipigia simu, wengine walivyosikia tu ndio wameanza kunilaumu bila kufanya uchunguzi na kunionya kwamba Wasanii acheni ulevi, watu wasianze tu kwa kulaumu’
0 comments:
Post a Comment