MIILI YA ASKARI WA JWATZ WALIOPOTEZA MAISHA DARFUR KUWASILI JUMAMOSI
Miili
ya askari wa Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Watanzania (JWTZ)
waliopoteza maisha Jimboni Darfur nchini Sudan kutokana na shambulizi la
ghafla itawasili Jumamosi wiki hii kwa ndege maalum katika uwanja wa
ndege wa Kimataifa wa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere. Kwa mujibu wa
taarifa iliyotolewa na Kurugenzi ya habari na uhusiano ya JWTZ imesema
mapokezi ya miili hiyo yatafanyika katika uwanja huo wa ndege majira ya
saa nne asubuhi.
Mara baada ya
kuwasili miili hiyo itapelekwa katika hospitali ya rufaa ya Jeshi Lugalo
na baadae utaratibu wa kuaga kwa heshima zote utatangazwa.
0 comments:
Post a Comment