MISS PROGRESS APATA AJALI MBAYA
Na Gladness MallyaMWANADADA ambaye ni Miss Progress International 2011/12, Julieth William amenusurika kufa baada ya gari lake kuacha njia na kuingia mtaroni alipokuwa akilikwepa gari lingine.
Akizungumza kwa shida kutokana na majeraha aliyoyapata, Julieth alisema ajali hiyo ilitokea Julai 8, mwaka huu maeneo ya Ubungo barabara ya kwenda Chuo Kikuu akiwa anaendesha gari lake aina ya Suzuki.
“Yaani gari halifai kabisa, liko polisi na ukiliona huwezi kuamini kuwa kuna mtu ametoka akiwa mzima, mimi nilikuja kupata fahamu niko nyumbani hata sikumbuki kilichotokea baada ya ajali ile,…
Na Gladness Mallya
MWANADADA ambaye ni Miss Progress International 2011/12, Julieth William amenusurika kufa baada ya gari lake kuacha njia na kuingia mtaroni alipokuwa akilikwepa gari lingine.
Akizungumza kwa shida kutokana na majeraha aliyoyapata, Julieth alisema ajali hiyo ilitokea Julai 8, mwaka huu maeneo ya Ubungo barabara ya kwenda Chuo Kikuu akiwa anaendesha gari lake aina ya Suzuki.
“Yaani gari halifai kabisa, liko polisi na ukiliona huwezi kuamini kuwa kuna mtu ametoka akiwa mzima, mimi nilikuja kupata fahamu niko nyumbani hata sikumbuki kilichotokea baada ya ajali ile, namshukuru Mungu sana kwani nilikuwa nife,” alisema Julieth.
0 comments:
Post a Comment