Wakati maelfu ha waumini wa dini la Kiislam duniani wakiwa ndani ya mfungo mtukufu huku wengi wao wakitumia kipindi hiki kupunguza maovu yao kwa mola kwa kufanya ibada,Hali imekuwa tofauti aliyekuwa mshiriki wa shindano la kumtafuta Miss Utalii Taifa Faithiya Madoud amepiga picha chafu za kujidhalilisha pamoja na kumdhalilisha mwanamke wa kitanzania.
Picha hizo chafu kwa mara ya kwanza zilinaswa toka kwa chanzo chetu cha habari ambapo inadaiwa msichana huyo ambae ameanza kuonja radha ya ustaa kufuatia kufanya vyema kwenye filamu za Mrembo wa Facebook na Nimpende Nani ambapo filamu zote hizo amecheza kama staa.
Habari za uhakika toka kwa chanzo chetu kilichofikisha cd nzima ya picha hizo mezani kwa mtandao huu hatari kwa kunasa matukio magumu kilisema kuwa msichana huyo ambae mapema mwaka huu alishiriki shindano hilo la Miss Utalii Taifa yaliyofanyika Mkoani Tanga. Lakini kwa bahati mbaya hakufanikiwa kushika nafasi za chini lakini alichaguliwa kuwa balozi wa Hotel zote za Kitalii nchini Tanzania pamoja na Kule Zanzibar
Hata hivyo habari zaidi ziliendelea kusema kuwa binti huyo kabla ya kuingia kwenye umiss alikuwa ni msanii maigizo na ametamba sana kwenye filamu hizo kiasi cha kujizolea umaarufu mkubwa nchini.
Aidha chanzo hicho kilisema picha hizo ambazo nyingine ni mbaya sana ambapo blog hii imeshindwa kuzitundika zote kwa kuzingatia maadili kwa wasomaji wetu lakini ilidaiwa kuwa picha hizo alikuwa anapigwa na mwanamke mwenzake na ilionekana walikuwa Hotel na haikufahamika walifika kufata nini kwenye nyumba hiyo ya wageni.
0 comments:
Post a Comment