Tuesday, July 23, 2013
Nilisoma naye chuo kimoja ( jina kapuni ), rafiki yangu alimpenda
sana huyu msichana, but she was pretending to be in love with another
man
( ambaye kwa mujibu wa taarifa za uhakika kutoka kwa watu
wa karibu na huyu binti, walisha mwagana tangu enzi za pontio wa
pilato and its like he was not existing ).
Jamaa kwa kuwa alikuwa
anamfeel huyu binti alienda naye hivyo hivyo kama mshika mapembe
hadi tukamaliza chuo mwaka 2008. Binti alikuwa anampeleka sana
jamaa, madesa yote yalikuwa ni wajibu wa jamaa, achilia mbali ishu
za kumfanyia takehome tests and all that...
Tumemaliza chuo, binti
yupo mjini na jamaa yupo mjini but msimamo wa binti ulikuwa
vilevile kwamba ana mtu wake toka zamani na wana mipango ya
kufunga ndoa, jamaa kapiga sana simu katuma sana meseji hadi
akachoka.
Mwaka huo huo (2008) jamaa akapata FULLBRIGHT SCHOLARSHIP,
akiwa marekani akatokea kupendana na dada mmoja chotara wa
kizungu, wamefunga ndoa na sasa hivi wana mtoto mmoja. Kwa sasa
jamaa ana fanya PHD kwenye chuo kimoja marekani ambako anaishi na
familia yake...
Mwezi uliopita alikuja kutembea home na
kumtambulisha mke wake. He is no longer talking about that gal. Sasa
kinacho nifanya nimshangae huyu binti, she is now blaming on us,
anasema sisi ndo tumemshauri jamaa aachane naye, mara ooh jamaa
alikuwa na maana gani kumtaka yeye kimapenzi halafu anakuja
kuoa mwanamke mwingine!!
I told her i dont have anything to do with
that plus nikamuuliza kuhusu the so called mchumba wake na hakuwa
na majibu yenye kueleweka but mwisho wa siku amejutia sana
mambo yote aliyo mfanyia jamaa, alijaribu kumuomba msamaha, jamaa
kamwambia yeye hana tatizo nae ila kuhusu uhusiano ndo hivyo
tena,yeye tayari ni mume wa mtu. Anafikisha miaka 30 mwaka huu,
hana mchumba wala bf, anauza dawa za GNLD ( U CAN SEE HOW
DESPERATE SHE IS )
KWENU MABINTI: Zile zama za SITAKI NATAKA , zimekwisha pitwa na
wakati, do not pretend to be in love with someone else wakati
unajua kabisa katika nafsi yako kwamba upo singo na unahitaji
mwanaume..Kumbania mwanaume kwa muda mrefu hakuwezi kuongeza
thamani yako hata kidogo.
0 comments:
Post a Comment