VAI WA UKWELI AMTAKA MUME WA AUNT EZEKIEL



KATIKA hali isiyo ya kawaida msanii anayechipukia katika filamu za Kibongo, Isabella Fransis ‘Vai wa Ukweli’ anamtafuta ubaya gwiji katika tasnia hiyo, Aunt Ezekiel kwa kusema anamtamani mumewe.

Isabella Fransis ‘Vai wa Ukweli’.
Vai wa Ukweli bila ya kupindisha maneno amedai kuwa hapati usingizi kutokana na kumzimia Sunday Demonte ambaye ni mume wa Aunt.
Akizungumza na mwandishi wetu, Vai alisema ili kuonesha kuwa anachokisema kinatoka moyoni mwake, amekata vipande vya picha za Dimonte na kuvibandika chumbani kwake.
“Kusema ukweli nampenda sana Sunday na sijaanza kumpenda leo wala jana kwani namfahamu tangu zamani alipokuwa Kariakoo,” alisema Vai.

Aunt Ezekiel.
Msanii huyo chipukizi alisema anamuonea wivu Aunt kwa kuamini kuwa anafaidi sana kwa kuwa na mwanaume huyo.
Kwa upande wake Aunt alishangazwa na taarifa hizo na akaomba atafutwe baada ya kumalizika kwa Mwezi Mtukufu wa Ramadhani ili ajue cha kufanya.
“Haya mambo ni makubwa jamani, sijawahi kusikia mtu akimpenda mume wa mtu na kusema hadharani, lakini ngoja nimalize Ramadhani, nitamtafuta aniambie vizuri,” alisema Aunt. Dimonte ni mume wa Aunt ambaye kwa sasa anaishi Dubai.

0 comments:

Post a Comment