Saturday, July 20, 2013
Wanawake wenye sura hii, huringia sana maumbile yao...!
Napenda
kutahadharisha kwamba, picha unayoiona hapo juu haihusiki moja kwa moja
na tabia nitakazozitaja kuhusu wanawake wenye sura kama hiyo. Sura
hiyo nimeiweka kama kielelezo tu.
Wanawake wenye sura kama hiyo unayoiona ni wanawake ambao kwa kawaida
hutamani sana kuwa na maisha ya uadilifu, lakini kuna kuzongwa na
saikolojia ya makundi ambayo huweza kuwaharibu sana. Ni wanawake ambao
wanapenda sana kufika mbali kimaisha.
Wana tatizo kubwa la kukosa kujiamini au kujiamini kupita kiasi, hasa
linapokuja swala la uzuri wa sura au maumbile. Kutokana na hali kama
hiyo, wanaweza kuvaa kihasara hasara au kuwa wajeuri bila sababu, ikiwa
tu ni njia yao ya kujitetea kutoka katika hisia za kutojitosha.
Ni wanawake ambao wanajua kupenda kwa nje, yaani wakimpenda mtu
huonyesha kumjali sana, ingawa kwa ndani sana wanapenda kuona wakilipwa
kwa kila wanalofanya kwa wapenzi wao, kwa kifupi ni kwamba wanapenda
sana fedha na matanuzi ya hali ya juu. Wanakereka haraka sana, hasa
kwenye tendo la ndoa. Wanapenda sana kuona kila wanalotamani wao kwenye
suala la tendo la ndoa linakuwa. Kwa hiyo mtu akiwaudhi kwa upande huo,
hukereke kupita kiasi.
Kwa kawaida, wana ufahamu wa kutosha na wanapenda kujifunza na kupata
mambo mapya. Huwa wanapenda kuonekana kuwa ni watu tofauti kwa
kujibainisha kiufahamu. Kama wana kipaji hujitahidi sana kukitumia kwa
lengo la kujibainisha kama wao na sio kama wasanii wengine.
Wanaweza kushindwa sana kudumisha ndoa zao kwa sababu ya kutojiamini
kwao ambako kwa wapenzi wao huweza kuita ujeuri au ujuaji. Lakini ukweli
ni kwamba, siyo wajuaji na wajeuri , bali wanaamini katika kile
wanachokiamini. Wana tatizo moja kubwa la kutojali sana kuhusu miili
yao, kwa hiyo masuala kama yale ya kushiriki ngono holela ni ya kawaida
sana kwao. Siyo ajabu kumkuta mwanamke mwenye sura kama hiyo, akiwa na
mabwana kadhaa na kushiriki tendo la ndoa bila kinga wala kujali kitu.
Kuna wakati hutumia miili yao kama chambo, hasa kama wana maumbile
mazuri ambayo kwa bahati nzuri kwao, hutokea kuwa nayo. Kama wana
makalio makubwa, kwa mfano, hujitahidi yaonekane ili kama mtu anavutika,
ababaike au ‘afike bei,’ kama ni lazima. Hata hivyo mara nyingi
hutaka tu kuwaumiza watu, kwani hufurahia pale anapopita na watu kuvunja
shingo ili kuwaangalia.
Ni wanawake ambao kama wamepata malezi mazuri, huwa na malengo makubwa
maishani. Kama wamepata malezi mabaya, huhangaika sana, ingawa bado ile
hali ya kuwa na malengo na kutaka kuyafikia huendelea kuwa nayo bado,
ingawa siyo kwa kasi kubwa. Ni wanawake ambao wanajua na kuamini kwamba,
ni wazuri sana, jambo ambalo wakati mwingine huwafanya kutenda mambo
yenye kuwavurugia sifa zao. Kwa kuamini kwao hivyo, hufikia mahali
wakajikuta wamezua mitafaruku na kuwafanya wapenzi wao kukerwa nao
kirahisi….
0 comments:
Post a Comment