Waumini wafunga kanisa na kumtimua pasta
Waumini wa kanisa la Kanunga Baptist eneo la Mukurwe-ini wakiwa nje ya
lango kuu la kanisa baada ya baadhi ya waumini kufunga lango hilo Julai
21, 2012. Picha/JOSEPH KANYI
Na JAMES NGUNJIRI
Imepakiwa - Monday, July 22
2013 at
07:37
Kwa Mukhtasari
Kulitokea
kizaazaa jana asubuhi katika kanisa moja eneo la Mukurwe-ini, Kaunti ya
Nyeri baada ya kundi la waumini kumtimua pasta wao na kufunga kanisa.
KULITOKEA kizaazaa Jumapili asubuhi
katika kanisa moja eneo la Mukurwe-ini, Kaunti ya Nyeri baada ya kundi
la waumini kumtimua pasta wao na kufunga kanisa kwa kufuli.
Baadhi ya
waumini wa kanisa la Kanunga Baptist, Ichamara, walichukua hatua huyo
wakimlaumu kasisi wao Bw Muriithi Mbote kwa kutowaletea maendeleo na
kuwaongoza kwa njia isiyofa
Ibada ya
asubuhi ilitatizika na ilibidi kundi la waumini wanaomuunga mkono Pasta
Mbote kuomba nje ya lango la kanisa kabla ya polisi kuwasili ndiposa
lango likafunguliwa.
Wapinzani wa
pasta huyo walikuwa wameweka mabango katika lango la kanisa yakiwa na
maandishi ya kumlaani huku tukio hilo likiwavutia wakazi waliokuwa
wakielekea makanisa mengine kwa ibada.
Kundi
linalompinga pasta huyo lilisema kanisa lao liko nyuma kimaendeleo
kuliko makanisa mengine eneo hilo na ndiyo sababu walitaka pasta huyo
ahamishwe.
Walimlaumu
pasta huyo kwa kuzuia baadhi ya vijana kujiunga na kamati ya kanisa,
wakisema alikuwa akiendesha shughuli za kanisa kwa njia isiyofuata
kanuni za kanisa zinazowapatia waumini mamlaka ya kufanya maamuzi.
“Pasta Mbote
amekuwa hapa kwa miaka 10 iliyopita sasa. Tunataka ahamishwe ili kanisa
letu lipate nafasi ya kustawi,” akasema Bw Antony Muturi, muumini wa
kanisa hilo. Hata hivyo, baada ya polisi kuingilia kati, makundi hayo
mawili yaliandaa mkutano mfupi kwa amani na waliofunga lango wakafungua
na kuruhusu ibada kuendelea.
Maandamano
Muumini
mwingine Bw Samuel Kamiri, alisema walicholalamikia waumini hao
hakikuhitaji maandamano, bali walipasa kuitisha mkutano na kamati ili
kusuluhisha tofauti zao kwa amani.
“Tunaanika jambo hili kwa umma kwa njia isiyofaa. Tunafaa kuketi kama wangwana na kutafuta suluhisho,” akasema Bw Kamiri.
Akizungumza
na wanahabari, Pasta Mbote alikanusha madai dhidi yake na kusema yuko
tayari kuhama kanisa hilo ikiwa waumini hawakutaka aendelee kuhudumu.
“Sina uwezo
wa kulazimisha jinsi kanisa linapasa kusimamiwa. Ni kamati ya kanisa
iliyo na mamlaka ya kufanya hivyo,” akasema Pasta Mbote.
Alisema kamwe
hakuwa na habari kuhusu mambo aliyolaumiwa na wapinzani wake kuhusu na
kuongeza kwamba amekuwa akihusisha waumini katika maamuzi ya jinsi ya
kusimamia kanisa hilo.
0 comments:
Post a Comment