Raia wa Brazili wanaomboleza vifo vya watu mia mbili thelathini na watatu waliofariki dunia katika ajali ya moto iliyotokea kwenye ukumbi wa muziki katika mji wa kusini wa Santa Maria.
Maafisa wanasema kuwa wengi wa waathiriwa walikuwa ni wanafunzi waliokufa baada ya kushindwa kupumua kutokana na moshi mkubwa.
Wengine zaidi ya mia moja wanapata matibabu hospitalini . Serikali ya Brazil imetangaza siku tatu za maombolezo . Taarifa zinasema kuwa moto huo ulianza wakati waimbaji wa bendi moja walipowasha fataki.
Maswali sasa yamekuwa yakiulizwa kuhusu usalama wa kumbui za starehe,
huku kukiwa na madai kuwa cheti cha huduma za zima moto kilikuwa
kimepitwa na wakati. Hili ni jana kubwa la moto kuwahi kuikumba Brazil
kwa zaidi ya miongo mitano
Familia za waathiriwa wamekuwa wakiomboleza juu ya majeneza za jamaa zao
katika ukumbi wa mamozezi ambao unatuimika kama jumba la kuhifadhia
maiti.
Kwa sababu ya heshima kwa waliofariki, serikali iliakhirisha sherehe
iliyotarajiwa kufanyika leo Jumatatu katika mji mkuu, Brasilia,
kuadhimisha siku 500, kabla ya kombe la dunia kungo'a nagna nchini humo
mwaka ujao.
Mazishi ya kwanza mjini Santa Maria yanatarajiwa kufanyika leo , kwa mujibu wa magazeti ya nchi humo.
Maafisa wa utawala wametoa majina ya waathiriwa hao,230 huku maiti watatu wakisalia kutotambuliwa.
Kulingana na taarifa za kituo cha televisheni cha Globo,wengi wa waathiriwa walikuwa kati ya umri wa miaka16 na 20.
Zaidi ya watu 100 wanapokea matibabu baada ya kushindwa kupumua kutokana na moshi mkubwa.
WABUNGE
waliochomewa nyumba na mali zao katika vurugu zilizotokea Mtwara juzi;
Anna Abdallah na Mariam Kasembe, jana waliangulia vilio walipotakiwa na mwananchi kuzungumzia tukio hilo.
Nyumba
za wabunge hao wa Viti Maalumu na mali zingine kadhaa za taasisi
mbalimbali, ni miongoni mwa vitu vilivyoharibiwa katika vurugu hizo
ambazo pia zilisababisha vifo vya watu wanne wilayani Masasi.
Akizungumza
kwa huzuni, Anna alisema hajui sababu za uharibifu huo, hasa
ikizingatiwa mwenyewe amekuwa huko kwa karibu siku tatu na hakuona
dalili za uhasama wowote dhidi yake.
Anna
ambaye pia ni Mwenyekiti wa Bodi ya Korosho alisema: “Nina siku ya tatu
hapa Masasi na nimeshiriki mkutano wa halmashauri kwa mwaliko na wakati
wote, sikuhisi chochote hivyo siwezi kujua sababu ya chuki iliyofanya
nyumba yangu ichomwe moto,” alisema.
Alipotakiwa
aeleze hali ilivyokuwa, alisema, “Wavamizi hao walipora kila kitu
nyumbani kwangu yakiwamo mapazia, kabla ya kumwaga petroli kila chumba
na kuwasha moto.”
Aliendelea
kueleza,” Kila kitu kiliteketea. Inatia uchungu kwani nyumba hiyo
niliijenga kwa kudunduliza fedha kidogo kidogo nikiwa mkuu wa mkoa.”
Anna
alisema, kundi hilo la vijana lilivamia nyumbani kwake saa 4:00 asubuhi
na kuanza kupora mali kwa kupita chumba kimoja baada ya kingine.
“Hali
si nzuri. Kila kitu kimeibwa na nyumba imechomwa moto, hakuna
kilichobaki. Walichukua kila kitu na itanichukua muda mwingi kujua
thamani halisi ya hasara iliyopatikana,” alisema.
Kauli ya Kasembe
Naye Kasembe alipokea simu ya mwandishi wa habari hii kwa kilio na kuikata huku akisema, “Jamani niacheni… Mwenzenu naumia…!”
Alipopigiwa tena baadaye, alisema anashangazwa na tukio hilo ambalo limemfika bila kutarajia na kumtia hasara kubwa.
“Wamepora
kila kitu katika nyumba na kuichoma moto, sijui atakuwa nani huyu,
kwani sina tatizo na wapiga kura wangu na sina mgogoro na mtu yeyote.
Nashindwa hata kuhisi nani kafanya uchochezi,” alisema Kasembe.
Alisema
wakati wa vurugu hizo, ndugu zake akiwamo mama yake, walikimbia na
kwenda kujihifadhi hotelini, lakini mpaka sasa hawajui wataishi vipi
baada ya nyumba hiyo kuteketezwa kwa moto.
“Jana
wanafamilia walilala hotelini na leo tupo nje ya gofu la nyumba yangu
ambayo imeteketea kabisa kwa moto, tunasubiri majaaliwa mengine, lakini
nimechanganyikiwa kwa kweli na sijui ni kitu gani hiki,
siamini,”alisema.
Polisi waeleza uharibifu
Watu 44 wanashikiliwa na polisi wilayani Masasi kufuatia vurugu hizo.
Kamanda
wa Polisi Mkoa wa Mtwara, Maria Mzuki alisema watu hao wamekamatwa kwa
wakituhumiwa kujihusisha na vurugu hizo zilizosababisha uhalibifu
mkubwa mali.