Friday, January 11, 2013
KOCHA MKUU WA SIMBA SIMBA PATRICK LIEWING
AKIWA NCHINI OMAN
KOCHA Mkuu wa Simba, Patrick Liewig amekomba mamilioni ya fedha kwa klabu hiyo kutokana na kusaini mkataba wa kuitumikia timu hiyo.Liewig, raia wa Ufaransa, alisaini mkataba wa miezi 18 akichukua nafasi ya Milovan Cirkovic raia wa Serbia aliyetupiwa virago na Wekundu hao kufuatia viongozi wa klabu hiyo kutoridhiswa na matokeo aliyoyapata katika mzunguko wa kwanza wa Ligi Kuu Bara.Uchunguzi uliofanywa na chokoza intertainment umeonyesha kuwa, Liewig atakuwa akichukua kiasi cha dola 6,000 (Sh milioni 9.6) kwa mwezi kiasi ambacho ni pungufu ya dola 2,000 ya kile alichokuwa akilipwa Milovan.Kabla ya kuondoka, Milovan alikuwa akiweka kibindoni kiasi cha dola 8,000 (Sh mil 12.7) kiasi ambacho uongozi wa Simba ulilazimika kumtafuta mbadala wake atakayeweza kupunguza gharama za mshahara huo.Hiyo ina maana kuwa, kwa miezi 18 Mfaransa huyo atachota kiasi cha shilingi milioni 172.8 huku Wekundu hao wakimpa nafasi ya kumuongezea ulaji huo endapo ataweza kufikia malengo ambayo timu hiyo inayataka.Hata hivyo, kiasi hicho ambacho Liewig anakipata Simba ni pungufu ya kile alichokuwa akilipwa katika Klabu ya EGS Gafsa ya Tunisia iliyokuwa ikimlipa kiasi cha euro 10,000 (Sh milioni 21) ambapo hakufanikiwa kudumu, kwani alitua Oktoba 2012 na kutimuliwa Novemba 2012.
0 comments:
Post a Comment