OPEN MIC YASHIKA
KASI DAR
Open mic ni ni mfano wa tamasha la kiburudani ambalo linakutanisha vijana na watu mbali mbali pamoja kwaajili ya kuonyeshana vipaji walivyonavyo na kuviendeleza zaid,utaratibu huu ni utaratibu wa muda mrefu sana katika nchi za wenzetu ingawa kwa hapa Tanzania ndio kwanza tunaanza nao.
OPEN MIC kwa hapa dar hufanyika kila baada ya alhamisi mbili kwa mwezi ikiwa ina maana ya kwamba inafanyika mara mbili kwa mwezi pale nyumbani lounge na hamna kiingilio unaruhusiwa kufika pale ili uweze kupata nafasi ya kuonyesha kipaji chako ulichojaliwa kama vile kuimba,kuigiza,kucheza,kutunga N.K
Baadhi ya watazamaji wakiangalia show zinazoendelea kwnye usiku wa OPEN MIC
moja kati ya wenye vipaji wakionyesha vipaji vyao kwenye usiku wa open mic
DHUMUNI KUU LA OPEN MIC
1) Kukutanisha vijana
2) Kukutanisha wasanii
3) Kukutanisha vipaji.
VIGEZO VYA OPEN MIC
1) Kujiamini
2) Uwe na ujumbe kwa hadhira
3) Uone ile ni fulsa yako ya kujitangaza na kupata marafiki wapya wenye tija
4)Uwe na kitu maalum ambacho unataka kukitoa kwa jamii
Raia wakishuhudia kipaji cha mtanzania mwenzao
Jitokeze sasa uwe ni miongoni mwa watanzania wanojitoa katika kuendeleza na kukuza vipaji vyao
0 comments:
Post a Comment