Jeshi hilo
limesema linawakamata machangudoa na kaka poa lakini wanapofikishwa mahakamani
wanapewa adhabu ndogo ikiwa ni pamoja na vifungo vya muda mfupi na kurudi tena
kuendelea na kazi yao hali inayovunja moyo jeshi hilo.
Kamanda mmoja wa
jeshi hilo ambaye hakutaka jina lake liandikwe gazetini kwa kuwa si msemaji wa
jeshi hilo, aliliambia gazeti hili kuwa kutokana na hali hiyo jeshi lake
limeamua kuchukua hatua hiyo ya kutoa kondomu ili wasiendelee kusambaza magonjwa
yanayosababishwa na ngono.
Mwanasheria wa
Kituo cha Haki za Binadamu (LHRC), Pecience Mlowe, alisema serikali inatakiwa
iandae sheria ya kuwashitaki machangudoa, na kuongeza kuwa mahakama kwa sasa
inatumia sheria ya uzururaji na ya kuendesha madanguro kwa ajili ya kuwaadhibu
watu hao.
Mlowe alifafanua
kuwa sheria zinazotumiwa na mahakama ni zile zilizorithiwa kwa wakoloni ambazo
haziendani na mazingira ya sasa, pia sheria zilizopo hazijafafanua kuwa
changudoa au kaka poa anaonekanaje, maeneo gani, kama ilivyo sheria ya wizi
inafafanua kuwa mtu akitoa kitu na kukiweka sehemu nyingine anachukuliwa kuwa ni
wizi.
Naye mmoja wa wasichana
anayefanya biashara ya kuuza mwili aliyejitaja kwa jina moja la Halima, alisema
polisi wanapowakamata, mara nyingine wanawadhalilisha kwa kuwalazimisha kufanya
nao
0 comments:
Post a Comment