kelly_rowland_120731_360


 Mwanamuziki wa Marekani aliyekuwa mmoja wa waliounda kundi la ‘Destiny’s Child’ Kelly Rowland alikuwa miongoni mwa kundi la abiria ambao ilibidi waokolewe baada ya boti binafsi walimokuwa wakisafiria kupoteza muelekeo baharini.
Muimbaji huyo nyota wa muziki wa RnB alikuwemo katika boti hiyo ya kukodi iliyokuwa ikiongozwa na boti nyingine ya kibiashara kuangalia nyangumi, ambapo nahodha wao alipoteza dira na kutoiona boti iliyokuwa ikiwaongoza hivyo kupoteza muelekeo.
Ilibidi walinzi wa Pwani kupewa taarifa na kutumia boti ya kuvuta ilitumwa kuiongoza boti hiyo binafsi kurudi kutia nanga.
Rowland na abiria wenzake walichukuliwa na kupelekwa Provincetown katika kingo ya Cape Cod, huko Massachusetts.