Nisha anawakaribisha watu wote kwenda kufuturu naye nyumbani kwake siku ya leo

Nisha anawakaribisha watu wote kwenda kufuturu naye nyumbani kwake siku ya kesho
Muigizaji Salma Jabu Maarufu kama Nisha ametoa mwaliko kwa marafiki zake wote na mashabiki wake wote kuungana naye nyumbani kwake maeneo ya kijtonyama kwa ajili ya kushirki naye kwenye futari maalumu aliyoindaa kwa ajili yao
Katika taarifa aliyoitoa kupitia mtandao wa kijamii wa instagram, Nisha amesema tofauti na watu wengi walivyokuwa wakisema kuwa futari hii ni maalum kwa marafiki zake tuu si kweli kwani ameandaa kwa mtu yoyote anayetaka kujumuika naye siku ya leo tarehe 21/07/2013.
Mwaliko wake kwa watu wote unasema….
"Naomba nichukue fursa hii kumkaribisha kila mmoja ambae atapenda kujumuika nasi siku ya kesho,ndugu yangu,shabiki wangu,rafiki yangu na kila mtu.ahsante sana .. nawapenda sana,Tujumuike pamoja kwa ajili ya Allah subhannallah wataallah RAMADHAN KAREEM.."

0 comments:

Post a Comment