Msanii
mkongwe kwenye tasnia ya afrika na kati Sintah amefunguka kuhusu
vitisho anavyopewa na msanii mwenzake wa muziki na maigizo Shilole kuwa
ajiandae kuchezea kipigo cha mbwa mwizi popote atakapomuona.
Akiongea
kwa njia ya simu toka nyumbani kwake Sintah baada ya mtandao huu kutaka
kueleza anachukuliaje vitosho hivyo vya Shilole ambapo alisema" Kaka
naambiwa sana na watu hasa wanaofatilia mitandao eti natafutwa kupigwa
na Shilole sasa ninacho shangaa huyo Shilole anapafahamu kwangu aje basi
anipige au kwenye ofisi zangu anapajua namkaribisha vizuri sana jamani"
Alisema Sintah
Aidha
Sintah aliongeza kusema kuwa" Mimi huwa sio mtu wa maneno yeye aje tu
anipige na sio kutangaza kwenye mitandao kuwa ananitafuta anipige hayo
mambo ya bifu siku hizi watu wanayachukulia upuuzi kutafuta pesa ndio
mpango mzima hivyo mimi namshauri Shilole kama underground wa sanaa
nchini aachane na bifu badala yake akazane kwenye mambo yake ya kutafuta
pesa kwa ajili ya maisha yake na familia kwani uzee unakuja" Alisema
Sintah Chanzo cha ugomvi huo ulitokana na Sintah kuandika habari kwenye mtandao wake kuwa Shilole hawezi kuimba na Jennifer Lopez wa Marekani bora hata Linah wa THT anaweza kufanya hivyo kwa hiyo Shilole aache kuidanganya jamii. Mtandao wa Sintah uliandika hivyo
Aidha Mashabiki mbalimbali hasa wasomaji wa kwenye mitandao wamemuunga mkono Sintah kuhusu kauri yake" Ni kweli jamani Shilole hawezi kuimba na Jennifer Lopez hayo ni masihara jamani kwenda marekani ndio aje kuongea ulojo kiasi hicho kwanza ikumbukwe kuwa wasanii wote wa tanzania kule Marekani hawajulikani hata, hasa kwa sisi tunaofatilia tunajia" Alisema mfanyabiasha wa kimataifa aliyejitambulishia kwa jina la Hamu Juma.
0 comments:
Post a Comment