RUNGU LA TCRA LAIKUMBA CLOUDS FM KIPINDI CHAO CHA PIGWA STOP


Makamu Mwenyekiti wa Kamati Maadili ya Utangazaji nchini, Walter Bgoya ( akizungumza na wanahabari leo jijini Dar es Salaam ukumbi wa habari Maelezo.

KAMATI ya Maadili ya Utangazaji nchini imevifungia vituo viwili vya radio pamoja na kukipiga faini kituo cha Clouds FM kutokana na kukiuka maadili ya utangazaji.

Vituo hivyo vya redio ambavyo vyote kwa pamoja vimefungiwa kutorusha matangazo yake kuanzia leo kwa miezi sita ni pamoja na Imani FM cha Dar es Salaam na  Kwa-Neema FM kilichopo mkoani Mwanza.

Akizungumza na waandishi wa habari leo jijini Dar es Salaam, Makamu Mwenyekiti wa Kamati hiyo, Walter Bgoya alisema Kituo cha Clouds FM kimetakiwa kufuta kipindi 
chake cha Jicho la Ng'ombe mara moja pamoja na kulipa faini ya sh. milioni 5.
Akifafanua zaidi Makamu Mwenyekiti huyo alisema vituo vya Imani FM na Kwa-Neema vimefungiwa kwa kosa la kufanya kazi zao kwa uchochezi jambo ambalo ni kinyume cha maadili ya tasnia ya utangazaji. Kituo cha Clouds FM kimetakiwa kutoanzisha kipindi kingine kinacho fanana na Jicho la Ng'ombe.

Kituo cha Imani FM kinadaiwa kufanya uchochezi kwa wananchi juu ya suala la sensa ya watu na makazi huku kile cha Kwa-Neema kufanya uchochezi juu ya mgogoro wa 
uchinjaji wanyama kwa Waislamu na Wakristu mkoani Geita.

Hata hivyo Kamati ya Maadili imeweka mlango wazi kwa vituo hivyo kukata rufaa endapo havikuridhika na adhabu vilivyo pewa kutokana na makosa vinao daiwa 
kufanya.
Kamati Imevitaka vyombo vyote vya habari kufanya kazi kwa kuzingatia Kanuni Sheria na maadili ya tasnia hiyo ili kuepuka kuzua migogoro kwa wananchi ambao wamekuwa 
wakiviamini vituo hivyo.
Hata hivyo mara baada ya ujumbe wa kamati hiyo kumaliza kusoma adhabu hizo kwa waandishi wa habari haukuruhusu maswali kwa waandishi wa habari, hivyo waandishi kubaki wameduwaa


STEVE NYERERE ASEKWA RUMANDE KWA KOSA LA KUSABISHA AJALI SOMA HAPA....



Picha hii inaonyesha Steve akipandishwa gari kuelekea kituo cha polisi.

Ajali hiyo ilitokea  wakati Stive akiwa na baadhi ya washiriki wa movie yake mpya  katika gari lake na wakiwa katika mwendo kuelekea eneo la kushuti sini zao, ghafla aliona gari aina ya funcargo ikiwa imesimama mbele yake huku katikati ya barabara akiwapo jamaa aliyekuwa akisimamisha magari katika eneo hilo.

Baada ya kushindwa kusimama kwa ghafla ndipo alipoigonga gari hiyo kwa nyuma na gari hiyo kutumbukia mtaroni.


Mashuhuda wa ajali hiyo walieleza kuwa chanzo cha ajali hiyo ni Fundi umeme aliyekuwa akisimamisha magari katika eneo hilo ili kuweza kuondoa waya wa Umeme uliokatika na kulala katikati ya barabara huku ukiwa na moto, ili kuepusha madhara zaidi.


Baada ya ajali hiyo, walifika askari Polisi wakiambatana na askari wa usalama barabarani, ambapo alianza kupima ajali hiyo huku madereva wakijibizana na fundi aliyesimamisha magari, ambapo majibizano hayo yaliingiliwa kati na mmoja kati ya askari waliofika eneo hilo.
Katika majibizano hayo baina ya fundi, Askari na madereva wote wawili, ndipo kulitokea kupishana kauli baina ya Steve na Askari huyo, aliyediriki kumuita Stive mjinga, ambapo Steve alishindwa kuvumilia na kuamua kumjibu na ndipo alipokunjwa Shati kaptula na kukokotwa hadi katika gari walilokuja nalo askari hao na kumpakia na kisha kuondoka naye kuelekea katika Kituo cha Mabatini.

Credit:Habari mpasuko 


SAMAKI ALIYEFANANA NA NGURUWE HUYU HAPA

 

HAYA NI MAAJABU..  SAMAKIHUYO AMBAYE ALONEKANA KUWASHANGAZA WENGI KUTOKANA NA MWONEKANO...!!



SABABU ZA DRAKE KUZUIWA NA MABAUNSA KUINGIA CLUB

Mtandao wa TMZ umeripoti kwamba rapper Drake alizuiwa kuingia kwenye club moja ya usiku huko Hollywood Marekani weekend iliyopita.
Sababu hasa ni kwamba hasimu wake, staa mwenzake ambae mwaka jana walirushiana chupa kwenye club moja ya usiku, mwimbaji Chris Brown tayari alikua ameshaingia ndani kwenye club hiyo hivyo mabaunsa walifanya kile walichoelekezwa cha kutoruhusu hizo sura mbili kuingia kwenye club hiyo kwa wakati mmoja.
.

Rihanna, Drake na Chris Brown, hii picha ilipigwa kabla hawajagombana.
Club nyingi sasa hivi zinahofia kuwaruhusu wawili hao kuwepo sehemu moja ili kuepuka yaliyotokea kwenye club waliyorushiana chupa ambayo ilifungwa kwa muda, pamoja na watu mbalimbali kudai fidia za kuumizwa kwenye ugomvi wa mastaa hao wawili ambao inaaminika ulikua ni wa kumgombania Rihanna.


CPWAA AJIPANGA KUKUZA VIPAJI VIPYA


wa miondoko ya muziki wa kizazi kipya Ilunga Khalifa Cpwaa anajipanga kwa ajili ya kuanzisha 'Academic' ili kukuza vipaji vya 'madensa' ambao wanaonekana kufanya kazi kubwa ya kupendezesha shoo za wanamuziki wa bongofleva

Aliyasema hayo jijini Dar es Salaam alipokuwa anaeleza mikakati ya kuibua vipaji vya madensa na jinsi ya kuviendeleza huku akiamini kuwa atakuwa ametoa mchango mkubwa wa kutoa ajira kwa vijana

Alisema kuwa kuanzisha kwa kundi hilo ni moja ya kutoa fursa kwa vijana ambao wenye uwezo na wamekosa nafasi ya kuonyesha vipaji vyao, na kujikwamua kimaisha kupitia vipaji hivyo

"Nampango wa kuanzisha darasa kwa ajili ya wacheza shoo tu itakuwa na mfanano wa kundi la THT kwani nia yangu ni kuwapa heshima na kuthamini mchango wa madensa ambao sasa wanatumika sana na wanamuziki wa bongo fleva" alisema Cpwaa

Pamoja na hayo aliongezea kuwa ili kuonyesha ana nia ya dhati ameanza na kundi la 'Choclate' ambao mpaka sasa wanafanya vizuri na wameweza kuibuka washindi katika mashindano mbalimbali ya 'danse'

Mbali na hayo Cpwaa alisema kuwa anakaribia kuachia video ya nyimbo yake mpya inayojulikana kwa jina la 'Mambo' ambapo sasa yupo katika hatua za mwisho kukamilisha video hiyo



Kutoka Facebook......
Joyce Dominick and 3 other people were tagged in Wikhalid Azizh Anzurooney's photo. — with De Love Junior and 8 others.
‎***tunarudi Ujana ***super model