ROMA MKATOLIKI:HASSO/ VIKWAZO/HARAKATI  


NA NINAVYOKUMBUKA AMBAVYO VILINITOKEA 


KATIKA MAISHA YANGU YA MUZIKI MIAKA YA AWALI 


NIKIWA NAANZA GAME!!!




1. MWAKA 2006 nikiwa tanga nilitoroka shule asubuhi nikamfukuzia B.TWELVE aliyekuja tanga nadhani kwenye show ya park lane!!am nat sure, nikamkuta ameshapanda bus na anasepa nikadandia bus namimi na kuanza kumtafuta miongonii mwa abiria, kipindi hiyo hata simjui kwa sura nikasema atakayekuwa brazameni tu humu ndani ndo yeye, huku bus linaenda niligonganishana naye macho akasmile nami nikasmile, nikamfata nikamkabidhi cd ikiwa na ngoma zangu 2 nilizirekodi kwa marehemu mr ebbo zamani sana motika!!!MUNGU AMREHEMU!!

"Braza ngoma zangu hizi pliz naomba kanipigie man zipo poa sana na tanga zimekubalika mno pliz kanipigie", akawa ananisisitiza poa zimefika kama kali zitapigwa we shuka uwahi shule maana bus llinazidi kwenda, nikashukia majani mapana kule kutokea stand!!!

Hazikupigwa zile ngoma na msoto ukaendelea kama kawa!! nadhani hazikuwa na kiwango bora au mm sikuwa mkali!!!!

2. MWAKA 2007 nilirecord ngoma yangu ya kwanza SALUTE kwa producer abbuy tanga studio za GOMBA RECORD, sasa wakati naileta dar kwa radio za huku nikameet tena na B.TWELVE akaniconnect kwa DJ NELLY ambae alikuwa mjengoni kipindi hicho kama mmoja wa mamusic department...

Basi nikafika mjengoni kitega uchumi pale mchana mapema sana nimeambiwa nifike saa kumi mimi nimefika saa tisa adabu za kale mbele hapo, kufika nje nikamwambia mlinzi nataka kumuona b.twelve nina ahadi naye, daah nilipewa mkwara huo miaka mia 8, nikaambiwa nikamngoje chini.

Sijakaa sawa mara bwana MATONYA naona anapita pale na anaingia ndani bila buguza kwa mlinzi, kidogo tena nikamuona A.Y naye akapita bila kuulizwa lolote, daaah moyoni nikawa natukana kimoyomoyo tu unajua zile.

Badae DOZEEN akatoka akanipeleka hadi kwa DJ NELLY, was like oyaa nelly mdogo wangu huyo msikilize...dahh jamaa akawa kama hasikii vile apo nimesimama na kacd kangu pembeni nashangaa tu kumbe huyu ndo GADNA na huyu ndo P.J okeeeii apo jahazi ndo inataka kuanza!!!

Nelly akaanza oya sema shida yako? nikajibu aaah blaza mimi naitwa ro....akanikata fasta oya una dakika 2 tu za kuongea namimi kisha akachukua cd akaiweka kwenye machine vile inaanza tu akaskip skip hapo yani kaisikiliza ngoma ndani ya sekunde 15 au 20 akaitoa cd na kunijibu hamna kitu production mbovu na huwezi kuchana!!! kisha akamgeukia gadna na kuendelea na hadithi zao, mi nikamuuliza asa bro nishauri nifanyaje? oyaa dogo tuna maongezi hapa huoni!!? hatuwezi kupiga ngoma kama hiyo akanijibu kwa ukali dah nikakosa pozi nikaanza kusepa, huku moyoni najisemea aah we gadna si ni mtanga mwenzangu wewe hata hutii neno kaka?

Nikamfata b. twelve wangu maana ndo alikuwa kimbilio langu mjini hapa, naye hakuwa na jinsi aise maana hawezi kupiga ngoma kama department haijaruhusu sema akanishauri nikairudie ngoma ile kwa DUNGA...kipindi hiyo dunga ni bad news aisee...

So nikatoka pale nikaipeleka ngoma ileile RADIO EAST AFRICA nikaiandikisha na nikasepa hapo nauli inaelekea kuliwa, babaako nikalirudisha kunani tanga moja...

Aaah east africa radio bana wakanipigia simu na kusema ngoma yako tunaitambulisha leo na wana segment inaitwa ipotezewe au iendelee kuwepo ki2 kama hicho...basi nikiwa tanga nikatega sikio kwenye satelite kusikiza badae wakaipiga na ikapata kura 338 zikisema iendelee kuwepo na kura 34 zikisema ipotezewe nakumbuka hadi leo hiyo!!! basi ngoma ikapita na ikawa inapigwa pigwa east africa radio!!

Wakati huo huo samahani kabla sijaenda tanga nikiwa dar nilikutana na JAFFARAI alikuwa ni rafiki wa karibu wa braza angu, braza akanitambulisha "huyu mdogo wangu anaitwa ebra au roma anarap na kaleta ngoma yake"...hapo natamni jamaa aseme tuisikize...(si unajua zile ukiwa unajiamini na ngoma kali!!)basi tukamshawishi aisikize, basi tukaenda kwenye gari na akaiweka...

Uwiiiiiiii jafarai akaanza "aaah mbona anachana kama mwana FA? aaah hana style yake huyu babu, tafuta style yako mzee, game gumu mzee, njoo kivyako man", asa nikawa najiuliza nachana vipi kama FA? mh nikaona ananikata tu nikamchana bro tusepe bana naona navurugwa tu!! tukaaga tukasepa kinyonge!!

3 MWAKA 2008 nimeshajichanga nipo fresh ndio nakuja dar rasmi sasa kurekodi TANZANIA hapo nimeshaongea na nahreal, na pia nakuja kuirudia ile ngoma iliyokataliwa radio nakuja kuirudia kwa dunga!!

Ndipo hapo tukiwa na braza mitaa ya mikocheni nadhani!! ndio tunakutana na FID Q, JAFFARAIi na MUSSA HUSSEIN wa uswazi yule, tukafika na bro hadi pale tukasalimia pale ila si unajua kisanii mara nyingi ukimsalimia mtu ni kama anakuwa anakukataa hivi anaitikia short short ndivo ilivokuwa.

So braza akaanza kuongea na jafarai mambo yao tu aaah katikati ndo wakachomekea braza akamwambia jaffarai "aah tunaenda 41 rec kwa dunga nampeleka mdogo wangu huyu si unamkubuka"?? jafarai akajibu aaah huyu si yule wa kipindi kileee? hapo ujue mwaka umeshapita hapo, braza akamjibu yeah ndo huyu sasa amekuja kuirudia ile ngoma huku kwa dunga!!

Jafarai akasema aaah amebadilika? au bado anachana vile vile? dogo badilika aisee game gumu sana dogo kwa style ile unapoteza hela tu huwezi kutoka, sasa akaanza kunivuruga tena ila moyoni nikawa nasema " mbona fid Q haununui huu ugomvi? yani kwanini haulizi lolote daah hapo FID Q kajikausha hata hatusikilizi yani yeye busy wanaongea na mussa tu, mi nikawa natamani blaza aseme kitu tu.

Hatimaye fareed akaingilia bana "oya kwani vipi bab? mbona kama unamnyea sana jamaa"? akamuuliza jafarai? jafarai akajibu "ah huyu dogo alikuja huku kama mwaka umepita hivii, akaniletea ngoma yake, ila ni ya kiwaki!! sasa kaenda kujipanga nw karudi rasmi...

Fid akasema niaje bab? unaimba au unarap? nikamwambia narap!! akasema ok 1,2,3 twendee...mamamammama ndo nilichokisubiri kwa muda mrefu hiki..

Nikaanza kuchana ngoma ile iliyokataliwa radio na iliyopingwa na jafarai...sasa kadri ninavyozidi kuchana naona jinsi bwana kubanda anavyozidi kunogewa, namm naongeza misifa hapo nachana tuu kwa hisia!!!

Ikawa poa sana kwake na akakubali hadi kuamka kwenye kiti na kunipongeza kuwa am good, lakini mooyni nikawa nataka nimchanie TANZANIA maana ndo nimekuja kuirekodi na ndo nina mzuka nayo na ndo naiona ni ngoma kali, yani zile za ( kama kadata nahii tu je tanzania nikichana itakuwaje)? so nikamwambia ngoja nikuchanie ingine...akakataa akasema aaah mi sitaki nyingine, nichanie hii hii iliyokataliwa...

So nikapita nayo tena. sasa ujuee na ngoma hiyo ninayochana hapa ndo baadhi ya mashairi yake yamepita tena kwenye MATHEMATICS na MECHI ZA UGENINI...niliyarudia koz sikutaka yapotee bure vitu kama "ndoto zangu kitambo zilikuwa nije kuwa padre, zikayeyuka nilipopuliziwa moshi wa weed etc.

Basi fid alikubali sana na hapo ndipo akasema una IQ sana bab...ndio chanzo cha ule mstari wa kusema "nawazidi kwa IQ shahidi fareed kubanda"!!! ambapo tazama sasa nimeuimba kwenye ngoma ya 4 toka niambiwe hivo nayeye!!!

Basi alikubali sana na akasema ni bora nikarudie kwa macko chali na akawa anampigia simu sema marco hakupatikana akaniachia namba yake, sasa jafarai nayeye alipoona fid anakubali akawa nayeye anasema aah dogo sasa amebadilika sasa hahaha moyoni nikawa na furaha sana unajua inavyokuwa unakubaliwa na watu kama hawa kwa kipindi hicho u knw it!! nikasepa na braza tukawaacha majamaa nikaendelea na hasso za kurekodi kwa dunga na nahreal!!!

HIZO NI BAADHI ZA MICHONGO ILIYOHAPPEN KABLA HAIJATOKA WALA KUREKODIWA NGOMA YA KWANZA YANGU ILIYONITAMBULISHA "tanzania"

4. BASI YAPO MENGI SANA YANAJAA KITABU NADHANI NA MENGI NI YA KUSISIMUA.

NATAMANIGI NIPATE INTERVIEW TENA YA TV AAAF NIHADITHIE KWA LISAA LIMOJA NA ZAIDI YOTE HAYA!!

SEMA YOTE HAYA UTAYAPATA KWENYE "DOCUMENTARY YA ROMA 2030" KUANZIA NAZALIWA HADI HAPA NILIPO SASA...

(UZURI NI KUWA KUNA BAADHI YALIREKODIWA SO ITAKUWA IPO REAL SANA)

TUENDELEE KUNGOJA!!! NAJUA MNAENJOY NIKIFUNGUKA HIVI

YAPO MENGI KAMA;

1. Mimi kukutana na kala na kugonganisha mawazo ya wimbo wa tanzania na wakwake wa wimbo wa taifa.

2. Nakaaya kunizingua kwenye kumshirikisha ktk ngoma yangu ya tanzania
, ila badae alinitafuta na kuniomba kolabo baada ya kutoka mathematics.

3. Wasanii wakubwa kunikatalia kwenye kolabo zangu kama mr president na tanzania, ndio maana nasimama bila kumshirikisha mtu kiivo.

4. Nikki wa pili alisababisha nikarekodi mechi za ugenini though yeye hajui hili.

5. Nilivyoingia kwa duke M. LAB na kurekodi mr president lakini haikutoka, namimi nikahamia tongwe na kuanza kurekodi upya hadi leo nipo tongwe.

6. Nilihit sana na tanzania lakini JAY MO aliwahi kuniambia hanifahamu... ila siku zikaenda akaja akanifahamu na tukafanya naye MVUA NA JUA REMIX kwa majani

7. Kwanini wadau wengi wakati natoka na tanzania hadi mr president walinambia DAT Z HIP HOP!!! safi kaza mwana aaaf leo inatoka hit kama mathematics wanasema sifanyi hip hop!! napayuka!! naropoka!! napiga makelele!! sina stye!!l na mengi tu hadi kusema tuzo sikustahili.... duuuh ATALI ATALI AISEE

8... NGOMA YANGU YA TANZANIA ILIVYOKATALIWA NA RADIO STATIONS NYINGI, ADAM MCHOMVU ALIKUWA MBISHI SANA THANX GOD AKAIPITISHA NA RADIO ZA MIKOANI ZIKASSUPORT MNO!!
..9.......10.....nth term
lav lav my pipo kuna vita kubwa sana zidi yetu basi katika sala zenu msinisahau kuniombea niwe na afya njema na maisha yenye heri na baraka na marefu mimi na familia yangu na tongwe wote na ndugu jama na marafiki wote!!!
mimi penda nyinyi apo!!!!

0 comments:

Post a Comment