SEREKALI YATANGAZA MAJINA YA WANAFUNZI WALIOCHAGULIWA KWENDA UALIMU





Serikali imetangaza majina ya wanafunzi 18,754 waliochaguliwa kujiunga na vyuo vya ualimu vilivyo chini yake ikiwa ni ongezeko la wanafunzi 1,659 ikilinganishwa na 17,095 waliochaguliwa mwaka jana.

Kati ya wanafunzi hao, 11,806 wamechaguliwa kusomea ngazi ya cheti (Grade A) na 6,948 watasoma katika ngazi ya stashahada.

Wanafunzi 363 wamechaguliwa kusoma elimu maalumu kwa ngazi ya cheti huku 57 wakisoma elimu hiyo kwa ngazi ya stashahada.

Akizungumza na mwandishi wetu jana, Msemaji wa Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Ntambi Bunyazu alisema wanafunzi wanatakiwa kuripoti kwenye vyuo walivyopangiwa kuanzia Agosti 15, mwaka huu.

“Usajili utafungwa Agosti 25 saa 12:00 jioni, ‘Joining instructions’ (fomu ya maelekezo ya kujiunga) zitatumwa kwa wahusika kupitia anuani zao.... fomu hizi pia zinapatikana kwenye tovuti ya Wizara ya Elimu na mafunzo ya Ufundi,” alisema.

Taarifa ya Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi iliyotolewa baadaye jana ilisema kuwa wanafunzi waliochaguliwa wanatakiwa kufika vyuoni wakiwa na vyeti halisi vya kidato cha nne na cha sita vinavyotolewa na Baraza la Mitihani la Tanzania (Necta) , ada ya muhula wa kwanza Sh100,000 au Sh200,000 kwa mwaka.

Wanatakiwa kuwa na “Sare ya chuo kulingana na maelekezo ya chuo husika, fedha za tahadhari chuoni na matumizi binafsi,” inasema taarifa hiyo.

Taarifa hiyo inaeleza pia kuwa wakuu wa vyuo wanatakiwa kuhakikisha wanafunzi wanaosajiliwa ni wale waliopo kwenye orodha iliyotolewa na wizara na si vinginevyo.

Wengi wa wanafunzi hawa ni wale waliohitimu kidato cha nne mwaka 2012 na kidato cha sita mwaka huu. Kwa upande wa wale wa kidato cha nne, matokeo yaliyotangazwa na Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi yalionyesha kuwa watahiniwa 159,609 wa shule walifaulu kwa daraja la kwanza mpaka la nne.

Inaonyesha pia kuwa kwa upande wa Tanzania Bara, wanafunzi 34,599 walifaulu kwa daraja la kwanza mpaka la tatu na kati yake waliochaguliwa kujiunga na kidato cha tano na vyuo vya ufundi walikuwa ni 34,213.

Kwa upande wa matokeo ya kidato cha sita mwaka huu, watahiniwa waliofaulu mtihani huo walikuwa ni 44,366 kati yao 40,242 wakiwa ni wa shule. Matokeo hayo yanaonyesha pia kuwa, watahiniwa 35,880 ndiyo waliofaulu kwa daraja la kwanza mpaka la tatu.

Kwa mujibu wa Kitabu cha Takwimu cha Wizara ya Elimu (Best), mwaka 2012 wanafunzi 17,095 walichaguliwa kujiunga na vyuo mbalimbali vya ualimu nchini.
Kutokana na takwimu hizo, kuna uwezekano mkubwa kwamba wanaokwenda kusoma ngazi ya cheti wanatoka kwenye kundi la wanafunzi waliopata daraja la nne.

Wanafunzi waliopata daraja la nne kwenye mtihani wa kidato cha nne mwaka jana ni 124,260.

Baada ya kutangaza majina ya wanafunzi waliochaguliwa kujiunga na kidato cha tano pamoja na vyuo vya ufundi, Naibu Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Philipo Mulugo aliliambia gazeti hili kuwa wanafunzi waliopata daraja la nne katika kiwango cha alama 27 watachaguliwa kujiunga na vyuo vya ualimu endapo wataomba.

“Vigezo vya kujiunga na kidato cha tano na vile vya vyuo vya ualimu ni tofauti. Kidato cha tano mwisho anatakiwa mtu mwenye alama 25 na masomo yake matatu yawe sawa, ualimu ni alama 27.

“Mwanzoni walikuwa wanakwenda wenye alama 28, lakini mwaka jana tukasema hapana, iwe alama 27 na tutachukua kuanzia waliomaliza shule mwaka 2008 kama wataomba, kwa sasa hivi watu wanaendelea na kazi ya kuwachagua,” alisema Mulugo.

Kwa muda mrefu, wadau wa elimu wamekuwa wakipiga kelele kuhusu wanafunzi wanaochaguliwa kusomea ualimu nchini wakitaka nafasi hiyo ichukuliwe na wale wanaofanya vizuri kwenye masomo yao.

MBUNGE WA CCM ANAYEDAIWA KUFADHILI MADAWA YA KULEVYA AJISALIMISHA POLISI



Mbunge wa Jimbo la Kinondoni, jijini Dar es Salaam kwa tiketi ya CCM, Iddi Azzan, aliyetajwa kwenye barua inayosadikiwa kuandikwa na wafungwa Wakitanzania waliopo Hong Kong “amejilisalimisha” kwenye ofisi za jeshi la polisi na kulitaka jeshi hilo lifanye uchunguzi dhidi ya tuhuma zilizoelekezwa kwake, ili hatua nyingine na ikibidi sheria, vichukue mkondo wake.

Azzan amesema alienda mwenyewe kutoa taarifa katika Kituo Kikuu cha Polisi Kati, jijini Dar es Salaam.

"Nimeamua kwenda kituo cha polisi kwa ajili ya kutoa taarifa ili ufanyike uchunguzi wa jambo hilo na ukweli ubainike  na hatua za kisheria zifuate juu yangu," alisema Azzan kwa njia ya simu



"Mimi sipo juu ya sheria ,  itakapobainika najihusisha na tatizo hilo, nichukuliwe hatua mara moja, na nitajiuzulu ubunge wangu," alisisitiza Azzan na kuongeza:


 "Wapiga kura wangu wa Kinondoni pamoja na wananchi kwa ujumla inatakiwa waelewe kuwa barua hizo zina nia mbaya zenye lengo la kunichafua na kama kweli wana ushahidi wangetaja majina yao," alinukuliwa Mbunge huyo.

MWANAMKE AOZWA KWA NGUVU NA KUBAKWA NA KUNDI LA WANAUME SIKU YA HARUSI...

Waandamanaji wakiwa wameshikilia mabango kulaani vitendo vya ubakaji.
Mwanamke wa India mwenye miaka 24 amelazimishwa kuolewa na kubakwa na kundi la wanaume kama adhabu ya 'heshima' baada ya kaka yake kutoroka na rafiki yake wa kike, imebainika jana.
Mwanamke huyo - ambaye hakuweza kutajwa kwa usalama wake - aliambiwa anatakiwa kuolewa na mume ambaye ni kaka wa mke wa mchumba mpya wa kaka yake kama 'kisasi' kwa uzinzi wa wawili hao.
Na ndani ya masaa kadhaa za kufunga pingu za maisha na mumewe mpya, akashambuliwa na kubakwa 'bila huruma' na kaka kadhaa wa mchumba wa kaka yake.
Kwa namna ya kushangaza, shambulio hilo ya kutisha lilidaiwa hata kupewa kibali na wazee wa kijiji hicho kilichopo makazi ya vijijini ya Uttar Pradesh, kaskazini mwa India, ambao walidai: "Jicho kwa jicho ni hukumu halisi."
"Ninakubaliana na uamuzi wao sababu ninajua kwamba kungekuwa na umwagaji damu katika kijiji hiki kama ningekataa kuolewa naye," mwanamke huyo aliwaeleza polisi.
"Mashemeji zangu walinibaka bila huruma siku hiyo hiyo niliyofunga ndoa. Ikawa utaratibu wa kawaida.
"Baba mkwe wangu alidai kwamba amekubaliana na ndoa yangu kwa vile alitaka kulipa kisasi (kwa familia yangu) namna hii."
Ajali hiyo mbaya imekuja kujulikana tu pale muathirika alipopata ujasiri wa kufungua madai hayo polisi.
"Machi 26, walifungua kesi dhidi ya kaka yangu na polisi walimkamata yeye na (mke wa mume wangu). Waliachiwa baada ya binti huyo kukiri mbele ya hakimu kwamba aliolewa naye kwa hiari yake," muathirika huyo alidai kwenye madai yake.
Baraza la kijiji au Panchayat, lilidaiwa kumlazimisha mwanamke huyo kuolewa baada ya kaka yake kuwa ametoroka na dada wa mumewe mtarajiwa mnamo Februari 15, mwaka huu.
Panchayat, ambalo liliketi ndai ya siku kumi baada ya kutokomea huko, lilitaka ndoa ya lazima. Mbali na hili, pia liliwataka wazazi wa mwanamke huyo kulipa Rupia 75,000 kama fidia kwa wakwe zake wapya.
Panchayat baadaye lilifafanua hali hiyo iliyojitokeza, likisema 'jicho kwa jicho ni hukumu halisi'.
Watuhumiwa hao wa ubakaji - wanafamilia wanaoshitakiwa -waliripotiwa kuweka bayana kwamba ilikuwa ni ulipizaji wao kisasi kwa kitendo cha utoroshwaji.
Mwanamke huyo kwa namna fulani alifanikiwa kukwepa majaribio yao ya kumkamata Julai 21, mapema asubuhi, na kufungua madai kwa polisi wa Muzaffarnagar mnamo Julai 27.
Mkuu wa polisi, Manzil Saini alisema: "Muathirika huyo amekutana nami. Kesi imefunguliwa chini ya Kifungu 376 ya IPC. Watuhumiwa watakamatwa hivi karibuni."
Kaka mkubwa wa muathirika huyo alidai uamuzi huo uliopelekea tukio hilo ulichukuliwa chini ya usimamizi madhubuti wa Panchayat.
"Polisi walitoa muda kwa watuhumiwa kuondoka kijijini hapo. Mume huyo wa chifu wa panchayat alikuwapo wakati tukio hilo la dada yangu likiamuliwa. Alikuwa msemaji mkubwa na kutaka adhabu kali mno dhidi yetu," alisema.
Mkuu wa panchayat alithibitisha uamuzi wake jana. Alidai aliwataka wafikie suluhisho la amani.
Tukio hilo limekuja wiki mbili baada ya mwanachuo mwenye miaka 20 kubakwa na kundi la wanaume na kisha kuchomwa moto huko Etawah, jimboni Uttar Pradesh, mkoa alikotokea Waziri Mkuu Akhilesh Yadav.
Katika kesi hiyo, kwa namna ya kushitusha, polisi hao si tu kwamba mwanzoni walikataa kufungua kesi lakini pia walionekana kukiuka wajibu wao wa kusimamia sheria na utii.

BAADA YA CLOUDS FM KUMWONGELEA MWISHO MWAPAMBA ,YE AKASIRISHWA NA KITENDO HICHO NA KUTOA TUSI ZITO LIVE


 Now ni clouds FM with Mwisho Mwampamba

WAKUTWA NA MAUTI WAKIFANYA MAPENZI.

Kwa Mujibu wa Ripoti iliyotolewa na wakazi wa eneo husika, inasemekana kwamba Bw. 

Mathias Nwoko,45, na Binamu yake Angela Ihuoma walifikwa na Umauti wakati wakiwa katika tendo la ndoa.
Wawili hao ambao asubuhi kabla ya kufariki walionekana pamoja wakicheza kwa furaha katika sherehe za kumkaribisha Padri Mpya katika Jimbo lao, Mathias ambaye ameelezwa alikuwa ndani ya ndoa kwa kipindi cha miaka 13 bila ya kupata mtoto alirudi na binamu yake usiku wakitokea kusikojulikana na kumkuta mkewe akiwa anaangalia T.V nyumbani kwake.
Mathias alimwambia mkewe atangulie kulala kwasababu yeye anachukua tochi amsindikize binamu yake huyo kwao. Mama mzazi wa Angela alipoona usiku unazidi na mwanawe hajarudi alimtafuta kupitia simu yake ya mkononi ambayo alipokelewa na Mathias akimwambia wapo pamoja.
Mpaka asubuhi, Si Mathias wala Angela Aliyerudi kwao na ndipo familia zote mbili zilipoingiwa na wasiwasi, Mke wa Mathias alienda katika nyumba yao ya pembeni asubuhi hiyo na ndipo alipowakuta wawili hao, mwanamke akiwa juu ya mwanaume.
Aliganda kwa muda asiamini anachokiona,hasa kuona wawili hao hawashtuki japo kawaona na ndipo alipogundua ya kwamba wamefariki Dunia. Ilibidi kutoa taarifa kwa familia ya Angela ambapo alikuja mama yake mzazi ambaye alipigwa na butwaa kutokana na picha iliyokuwa mbele yake.
Miili yao ilitenganiswa na kupelekwa hospitali huko Ogbor Nguru, jimbo la Aboh Mbaise.

Source:Global publishers

Kahaba anusurika kifo. Apigwa kikatili na wenzie wakidai “anauza” bei rahisi na kuwaharibia soko

Kahabaz



Kahaba mmoja katika mji wa Naivasha, jimboni Rift Valley, Kenya alinusurika kufa baada ya kupewa kichapo cha mwizi na makahaba wenzake kwa sababu wamekerwa na kitendo chake cha kuuza ngono kwa bei rahisi na kuwaharibia soko. Wenzake hao wenye hasira walimtwanga kwa mangumi na mateke, wakimshutumu kwa kutokuwa na ushirikiano na “kuharibu soko” hasa ukizingatia ilikua ni kipindi cha mwisho wa mwezi, ambapo wateja wamejaa mkwanja na mahitaji ya kununua ngono yameongezeka.
Wakati wakimpa kichapo, walitaka kumkeketa (kumtahiri mwanamke) kwa kutumia chupa iliyovunjika “ili iwe funzo” lakini akaokolewa na walinzi wa usiku (wengi wao ni wateja wake) kabla hajafanyiwa kitendo hicho.
Msuguano ulianza mwezi uliopita pale msichana huyo mwenye umbo nyororo na la kuvutia alihamia mitaa hiyo kitu ambacho kiliwakera makahaba wazoefu hapo maana walimuona kama tishio kutokana na urembo wake.
Kwa mujibu wa dereva wa bodaboda anayeitwa Peter, kahaba huyo amekua ni kivutio na anayependwa na wengi kutokana na uzuri wa umbo lake na rangi nyeupe ya ngozi yake. Zaidi ya “kupunguza bei,” inadaiwa kuwa kahaba huyo pia anatoa “huduma” kwa mkopo, kitu ambacho wenzie hawafanyi, hivyo kuzidi kuwaaribia biashara zaidi.
“Kwa kawaida, bei ni kati ya Ksh 100 mpaka Ksh 500 (kama TZ Shs 2,000 mpaka 10,000) inategemeana na mteja. Lakini “Brownie” anauza kwa hata Kshs 50 (TShs 1,000)” alidai Peter.
Idadi ya wateja wake ilikua kwa wingi na kwa kasi, kitu kilichopelekea wivu na chuki kutoka kwa makahaba wengine, ndipo walipofikia uamuzi wa kufanya njama za kupanga kumpa kichapo “ili iwe fundisho.”
Makahaba hao walitekeleza lengo hilo pale walipomzingira kwenye kona, gizani akiwa peke yake, na kumshambulia kikatili.
“Kwani unafikiria sisi tutakula wapi kama utaendelea kujiuza hii bei hasara.” Mmoja wa wanawake hao alimkaripia kwa sauti ya juu.
Kahaba huyo alipiga mayowe na kuomba msamaha kutoka kwa wanawake hao wenye hasira wakati anashambuliwa, ndipo walinzi waliposikia na kukimbilia kumuokoa.
Walinzi hao walipofika, walikaripiwa na makahaba hao wakiambiwa kuwa hiyo ni ishu ya wanawake, na wao haiwahusu.
““Unajua huyu mama huwa ananipatia kwa mkopo siku ninazokuwa nimechacha hivyo siwezi muacha auliwe na hawa mikora” alisema mmoja wa walinzi hao wakati wakijaribu kumuokoa mwanamke huyo.
“Wateja” wake wengine wakaingilia kumuokoa kahaba huyo ambaye alikua ameumizwa vibaya, na kumkimbiza hospitali.
Inaonekana makahaba wazoefu maeneo hayo wanatawala “ngome” yao na lazima wakatiwe panga na makahaba wapya, ambao lazima wajitambulishe kabla ya kujiunga kwenye “soko” lao.
“Brownie” bado yuko hospitali akipatiwa matibabu huku wateja wake wakimsubiri apone, ili waendelee kupata “huduma” zake kwa bei nafuu, na kwa mkopo.
“Maisha imekuwa ngumu sana na bei ya kila kitu, hata ya hawa wasichana imepanda sana. Tunaomba serikali iingilie kati ,” mmoja wa walinzi hao alilalamika.

AKAMATWA AKIFANYA MAPENZI NA MIFUPA YA MWANADAMU, ADAI ANA MAHABA MAKUBWA NA MAITI




Mama mmoja mwenye umri wa miaka 37 ameshitakiwa nchini Sweden kwa kufanya mapenzi na mifupa ya maiti.
Mama huyo pia alipatikana na makala aliyoaandika akifurahia kuwa mtu wa kwanza kufanya mapenzi na mifupa ya mtu aliyefariki dunia zaidi ya miaka 50 iliyopita.
Mkuu wa mashitaka Bi Kristina Ehrenborg-Staffas ameliambia shirika la habari la Reuters kuwa bibi huyo anakabiliwa na mashitaka ya kuvuruga amani ya marehemu.
Lakini mama huyo amejitetea akisema haoni kama amefanya kosa kwani anafurahi kufanya mapenzi na maiti.
Wakati alipokamatwa alipatokana akiwa na mifupa ya binadamu,mafuvu, na viungo vyengine.
Pia aliptikana na picha za vyumba vya maiti na makaburi.
Bibi huyo anasema ana mahaba makubwa na maiti.

Jamaa amuua mwanawe na kunywa damu yake,

JACKLINE WOLPER AMPA MAKAVU ALIEMUITA YEYE KAHABA ANAEJIUZA


 
Msanii  nyota  wa  filamu  bongo, Jacqueline Wolper   amewataka  wasanii wa  bongo  movie  kuacha  tabia  ya  kupigana  majungu  ya  kinafiki  ambayo  huchangia  kujenga  bifu  za  kijinga....

Akiongea  na  mpekuzi  wetu, wolper  alidai  kuwa  kuna  mipaka  ya  watu  kuishi  lakini  kuna  baadhi  ya  wasanii  wanaamini  kwamba majungu  ndo  mshahara  wao  kiasi  kwamba  wasipomsengenya  mtu  basi  hawawezi  kuishi...

Wolper  anadai  kuwa   yeye  ni  miongoni  mwa  wasanii  wanaosemwa  sana  kwa  mabaya  hasa  kuhusu  maisha  yake  ya  kila  siku.Hali  hiyo  inatokana  na  umaarufu  alionao  ambao  huwafanya   wasanii  wenzake  wamchukie  hasa  wasanii  wa  kike...



  Hii  ni  kauli  ya  Wolper  alipoongea  na  mpekuzi:


"Wasanii  tungekuwa  na  ushirikiano  kama  nisha  tungefika  mbali  sana.

"Mimi  simuogopi  mtu  katika  maisha  yangu, lakini  ninachohitaji  katika  maisha  yangu  ni  Heshima.

"Ukiona  nimekukwaza, basi  njoo  nyumbani  au  nambie  nikufuate  ili  tuyamalize  kibinadamu  na  si  kudhalilishana  mitandaoni...

"Kuna  msanii  mmoja  wa  kike  amekuwa  akinichafua  sana  mitandaoni   kwa  kuniita  kahaba, najuza  na  matusi  mengine  kibao.

"Huyo  ni  mtu  anayetafuta  pakutokea, anatafuta  kujulikana  kupitia  Wolper  na  pengine  kafulia  na  sasa  anatafuta  mtaji.

"Tangu  anitukane  sikuona  haja  ya  kumjibu  kutokana  na  heshima    niliyo  nayo  katika  kazi  yangu  na  heshima  yangu  kwa  wazazi , ndugu  na  jamaa.

"Niliamua  kumwachia  mungu.Kama  ni  kahaba  au  najiuza, mungu  anajua.Alisema  Wolper 

PICHA YA SUPER STAR OPRAH WINFREY AKILA BATA BONGO!!

oprah


A group of giraffe is called a “journey” There were 16 of them couldn’t fit in one shot

Kero za watoa huduma kwa wateja


Unapokuwa mtoa huduma kwa wateja (customer care) unatakiwa kuwa sharp, kauli nzuri na tabasamu kwa watu unaaowahudumia.

Hii imekuwa tofauti kwa watoa huduma wengi hapa Tanzania sijajua huko sehemu nyingine. Unafika sehemu unapokelewa na uso umekunjwa na majibu ya nyodo hasa ukiwa mrembo na mtoa huduma ni mwanamke! Wengine watu wanasubiri huduma mf; benki yeye anaongea na simu kwa mapozi yaani hana habari wala hajali ile foleni mliyopanga kumngoja yeye.


Wakati mwingine unaulizia huduma unahitaji maelezo ya kueleweka ila jibu utalopewa unaweza kukaa chini ulie! wanajisahau kama ile ni kazi inayomlipa mshahara na anatakiwa aitumikie.

Tubadilike jamani kama unahusika kutoa huduma kwa wateja unatakiwa uwe mkarimu,hujui unaye mfanyia nyodo ni nani au mnaweza kukutana wapi siku za usoni na wewe ukahitaji msaada wake maana unaweza kumjibu hovyo mkweo.Tunaishi kwa kutegemeana kama binadamu kwa hiyo kukaa mapokezi au kuwa customer care kusikuvimbishe kichwa ukajiona umefika.

Maboss nao wanatakiwa wawe makini na watu wanaowaajiri kwa ajili ya huduma hizo. Pia uanpoletewa malalamiko na wateja ili kulinda heshima ya ofisi yako unatakiwa uyazingatie na kuyafanyia kazi.Kwa leo naishia hapa inaowahusu ujumbe wamepata.

Wauza 'Unga' waliokamatwa Hong Kong wataja maboss zao yupo na mbunge maarufu


Mbunge Wa Serikali ya Jamhuri ya Muungano Wa Tanzania ametajwa na wafungwa wa kitanzania waliofungwa jela huko nchini Hong Kong kuhusika na biashara ya madawa ya kulevya.

Taarifa hiyo iliyomhusisha Mbunge huyo na mtandao huo mkubwa wa biashara hiyo ya madawa ya kulevya nchini Tanzania, ilitolewa katika barua maalum iliyoandikwa na mmoja wa Wafungwa katika magereza ya nchini Hong Kong ambapo inasemekana kuna wafungwa wa kitanzania wanaofikia 200.

Kati ya hao wafungwa 200 waliopo magerezani na vizuizini, 130 tayari wameshahukumiwa na 70 bado wanasubiri kesi zao kutajwa. Kuanzia Mwezi wa Tano mpaka wa Sita mwaka huu wa 2013, tayari Watanzania wapatao 50 wameshakamatwa na madawa ya kulevya wakati wakijaribu kuingia katika viwanja vya ndege vya nchi za China na Hong Kong.
 
 





Mbali na Hong Kong, pia kumekuwepo na taarifa mbalimbali za raia wa Tanzania ambao wamekatwa na madawa ya kulevya nchini Afrika ya Kusini na kwingineko duniani. Mmoja kati ya waliokamatwa na madawa hayo ni mwanadada mahiri wa Kitanzania ambaye alikuwa mrembo katika video mbalimbali za Bongo Flava anayeitwa Agnes Gerald au kama anavyojulikana na wengi kwa jina la Masogange.

Waraka huo wa mfungwa huyo wa Kitanzania pia umeorodhesha idadi kubwa ya wafanyabiashara wengine nchini Tanzania ambao ni wahusika wakubwa katika biashara hii haramu ya madawa ya kulevya.

Madawa hayo ya kulevya yanasemekana yanaingizwa nchini Tanzania kwa wingi kwa njia ya meli na boti mbalimbali yakitokea katika nchi za Pakistan, Afghanistan na nchi nyingine za Mashariki ya mbali.

Ni muhimu kwa serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kuanzisha kampeni kubwa ya kuwakamata wahusika wote katika biashara hii na kuwafikisha katika vyombo vya sheria, athari za madawa hayo zimezidi kuonekana sehemu mbalimbali nchini Tanzania na dunia nzima.

DIAMOND PLATNUMZ AENDA SHULE SOUTH AFRICA KUONGEZA VIDATO



The Bongo Flava Prince, Diamond Platnumz yupo nchini Afrika Kusini alikoenda kuongeza vidato kidogo. Apparently, hitmaker huyo wa Kesho amejiunga na chuo ambacho hakijajulikana jina lake bado na hajasema ameenda kusoma nini.

Kupitia Facebook, staa huyo amewauliza mashabiki wake wabashiri ameenda kusoma nini chuoni hapo na haya ni baadhi ya majibu.

Faiso Yahya: Ka si english course basi unenguaji

Galus de Focus: HOTEL MENEGEMENT

Benjamin Osarya Jr.: Unasoma matangazo….kwenye notes board.

Nelson Choka: Samahan form 4 umemaliza ww et..!! Labda una risit dogo mh

Rose Selestini: Unatafuta wadada wa chuoni.

Christian Biseko: wa kusoma uwe wewe??? Elimu siyo mchezo wewe!!!

Gara B Kubwa: English Course ili Ushiriki BBA mwakani…una Mbwembwe dogo wewee..

Emmanuel Makaga: Unasomea jnc ya kubun skendo mpya kwny mass media

Gabrie Lbrighton: Wanaosoma hawajitangazi wew may be ungetuambia akitoka huyu mwanamke uliye nae nani anafata.
Nàdhifá Dórnald Unasomea mapenz maana unayapenda sana.

VIDEO: Nando atimuliwa BBA kwa kuficha silaha na kutishia wenzie

WANAWAKE KUTEMBEA NUSU UCHI, KUMBE WANA LAO JAMBO


Kuna wakati wanaume hudhani kwamba, wanawake wanaovaa nusu uchi huwa wanafanya hivyo kwa sababu ya kutafuta soko kwa wanaume. Inawezekana kukawa na wale ambao wana sababu hizo, lakini wapo wale ambao wanalipa fidia kutokana na kuamini kwao kwamba, sura zao zimewaangusha, hivyo miguu yao mizuri inabidi kuziba pengo au udhaifu huo.

Wakati mwingine hata wanawake wanaodhani au kudhaniwa kuwa ni wazuri, wamekuwa wakivaa nguo fupi zinazoonyesha maungo yao. Hawa nao ni lazima wanalipa fidia ya kasoro fulani waliyo nayo. Inawezekana wameshindwa kulinda ndoa zao, au inawezekana hawajaolewa na sasa wanataka kuonyesha kwamba, pamoja na kutoolewa kwao, bado wao wana sura na miguu au miili mizuri.

Udhaifu wowote ambao unamkera mwanamke iwe ni wa moja kwa moja au kupitia nyuma ya ubongo wake, unaweza kuonyeshwa kwa mwanamke huyo kuyatangaza yale maeneo ya mwili wake ambayo anaamini ni mazuri. Kuyatangaza huko humpa ahueni kwa kuamini kwamba bado anayo thamani, kwani ataangaliwa sana na wanaume, kusifiwa na pengine kutongozwa.

"NIKIKUTA NINA VIRUSI VYA UKIMWI NI LAZIMA NIJIUE MAANA SIPO TAYARI KUCHEKWA".....




Msanii  wa  filamu  bongo,Baby Madaha  amefunguka  kwamba  siku  akianza  kuona  dalili  za  ugonjwa  wa  UKIMWI  ndani  ya  mwili  wake   atakunywa  sumu  kwa  kuhofia  kuchekwa  na  jamii.

Akiongea  na  mwandishi  wetu,Madaha  amedai  kuwa  kwa  sasa  anaamini  hana  ngoma  maana  siku  zote  hutumia  Kinga (kondom)   ili  asiambikizwe  gonjwa  hilo  japo  hana  uhakika  asilimia  zote  maana  hiyo  ni  mipango  ya  mungu.

"Siukatai  ugonjwa  huo  kwa  kuwa  sijui  ni  lini  naweza  kuupata  hasa  ukizingatia  kwamba  mimi  bado  ni  kijana  mbichi  ambaye  bado  nahitaji  kuifurahia  dunia"...Alisema  Baby Madaha..

Katika  mazungumzo  hayo, Madaha  anadai  kwamba  mpaka  sasa  hakuna  mpenzi  wake  yeyote  aliyekufa  kwa  Ngoma  ingawa  wapo  waliofariki  kwa  maradhi  ya  kawaida  na  ajali....

"Nikijua  tu  nina  ngoma  ni  lazima  ninywe  sumu  ili  kukwepa  balaa  la  wabongo.Najitahidi  kujilinda  ili  nisiudake  mapema"..Alisema Madaha  

Madaha  anadai  kwamba  kitendo  cha  yeye  kujiua  mapema  kitasaidia  kuwaondolea  wasiwasi  wasanii  wenzake  ambao  wataanza  kujiuliza  maswali  mengi  kuhusu  watu  aliowahi  kutoka  nao  kimapenzi

"Nitawasaidia  wasanii  wengine  ambao  nimewahi  changia  nao  mabwana.Najua  wataumia  sana, lakini  ndo  hivyo  tena, hakutakuwa  na  jinsi.

"Sijasema  nina  UKIMWI,Hapana,nimesema  kwamba  ikitokea  maana  watu  hawakawii  kupindisha  maneno"..Madaha

JIWE LA AJABU NCHINI TANZANIA NA HAIRUHUSIWI KULIPANDA WALA KULISOGELEA!! KWANI NI HATARII



 
Haya ndio maajabu ya Jiwe la Mbuji Wilayani Mbinga Mkoani Ruvuma
Maana ya neno Mbuji ni "Kitu kikubwa"

1. Ni jiwe pekee kubwa Mkoani Ruvuma,

2. lina vyanzo vingi vya maji chini yake,
 
3. Ni ngumu kulipanda na ukithubutu yatakayokukuta ni
juu yako na tayari Mzungu mmoja kapoteza maisha'

4. Ni ngumu kulizunguka,

5. Hutumika kwa matambiko kwa baadhi ya koo,

6. Kuna watu maalumu wanaotoa maelekezo kwa yeyote
anayetaka kulifikia ama kupanda,

7. Ni kivutio kikubwa kwa wageni wachache ambao
hutembelea Litembo, Maguu, Hagati nk huko Mbinga,
8. Linaheshimika sana na wakazi wanaolizunguka jiwe
hilo,
9. Sehemu kubwa ya watu wananchi wanaolizunguka
hawajawahi kulipanda wala kulisogelea kwa hofu,
10. Jina la jiwe hilo ndilo jina la Tarafa ya Mbuji wilayani
Mbinga.

SIJAWAHI PIGA PICHA ZA UCHI..,NIMEMFAHAMU SINTAH KUPITIA SKENDO YA KUGAWA PENZI KWA NATURE,RAYUU AFUNGUKA TENA....



Bongomovies.com imefanya interview kwa njia ya simu na mwanadada msanii Rayuu alaice Bungenzi kuhusiana na mambo mablimbali yanayoandikwa kwenye mitandao na tovuti mbalimbali nchini. 


Katika interview hiyo waliweza kupata mambo manne  kama  ifuatavyo:

  
 
1. Hajawai kupiga picha za utupu na kuzisambaza ili kupata umaarufu
 

Akiongea kwa msisitizo Rayuu amesema kuwa hajawai kupiga picha za utupu na kuzisambaza kwenye mtandao kwa ajili ya kupata umaarufu.
 

“Sijawai kusambaza picha za utupu ili nipate umaarufu, hizo picha kweli ni zangu na ukizitazama vizuri sio picha za utupu kama watu wanavyosema(?????), ni picha nilizopiga kwenye simu yangu kujiangalia tattoo yangu niliyochora kiunoni lakini kuna marafiki zangu waliochukua simu yangu na sijui ni nani ndio zilisambaa kutokea hapo na kila mtu kuandika stori anayoijua yeye” Alisema.
 


2. Hafahamiani na wala hajawai kuonana na sintah kwa zaidi ya miaka mingi sana


Rayuu amesema kuwa hajawai kuonana na sintah, wala hafahamiani naye personally na huwa anashangaa sana kwanini mwanadada huyu anamchafua kwenye blog yake.
 

“Kiukweli mi sifahamiani na Sintah, na wala hatujawahi kuonana kwa kipindi kirefu sana, sasa huwa nashangaa kwanini ananichafua na kunitukana kwenye blog yake. Kuna kipindi nilichoka nikaanza kumjibu lakini baadaye nikaona ni utoto bora ninyamaze kwanza nione kama ataacha lakini nashangaa hakui.
 

Huyu dada mi huwa simuelewi kwakweli,anagombana na kila mtu, nahisi anaweza kugombana hata na panya. Kwanza ni mtu mzima sana kwangu. 


Nakumbuka mi nimemfahamu yeye wakati teyari kashakuwa maarufu na skendo za uroda kwa Juma nature na mimi nilikuwa bado mdogo sana. Sa sijui kwanini hakui. Kila siku anatukanwa kwenye blog yake lakini wala hajali.”…Alisema Rayuu
 

3. Marehemu Mzee Kipara ndiye haswa aliyemuingiza kwenye sanaa
 
Watu wengi hawajui kuwa marehemu mzee kipara ndiye aliyemuingiza Rayuu kwenye sanaa. Rayuu alisema kuwa anakumbuka siku moja kundi la kaole walienda kurekodi igizo  lao mitaa ya nyumbani kwa kina Rayuu na alipowaona alimfuata mzee kipara na kumueleza nia yake na ndipo alipompeleka na kumtambulisha kwenye kundi la kaole na kuanza kupata nafasi ya kuigiza na kufanya mazoezi kundini hapo.
 

4. Sio mtu wa kutoka sana na akila "bata" anaumwa sana kesho yake
 
Rayuu amesema yeye sio mtu wa kutoka na kupenda kwenda club kama wengi wanavyodhani bali hupenda sana kushinda ndani kwani akifanya hivyo kesho yake lazima aumwe siku nzima.

Mwanamke Mwenye Matiti Matatu Kifuani (PICHA)


Bolt Aingia Kwenye Uwanja wa Queen Elizabeth na Gari la Injini ya Rocket


Daktari Aliyempa Michael Jackson Vidonge Vilivyosababisha Kifo Chake Kuwa Huru Mwezi Oktoba


Marehemu Michael Jackson
Dr. Conrad Murray anatagemea kuwa huru toka jela itakapofika mwezi October. Daktari huyu alikutwa na hatia ya kumpa dawa ambazo zilichangia kupelekea kifo cha aliyekuwa nyota wa muziki wa pop Michael Jackson.

Daktari wa Michael Jackson anatategemea toka jela katika kipindi cha miezi mitatu ijayo, wakili wake alisema.

Conrad Murray anategemea kuwa mtu huru mnamo Oct. 28 ambapo ni chini ya miaka miwili toka alipofungwa kutokana na kumpa aliyekuwa nguli wa muziki wa pop Michael Jackson dawa zilizopelekea kusababisha kifo chake.


Murray, 61, alikutwa na hatia na kutumikia kifungo hicho mnamo mwezi November 2011.

CHRISS BROWN AJARIBU TENA KURUDIANA NA RIHANNA-AMFUATA FUATA



Chris Brown & Rihanna have broken up since May but Chris might be trying to patch things up



He Tweeted that he's in Geneva to 'clear his head', which just so happens to be in the same part of the the world where Rihanna is now on her Diamonds World tour.

Chris also wrote "Sometimes you just need that time to get away and think about life." So don't be surprised if you see pictures of Chris Brown and Rihanna together soon...:-)..

VIDEO:MAHABA WANAOJIPANGA KUWACHUNA WAKULIMA KIPINDI CHA MAVUNO

VIDEO:Lulu na Mama Kanumba wakijiachia na nyimbo za go...

MASOGANGE BALAA JIPYA

Shakoor Jongo
HUKU  akiwa hajui nini hatima ya kesi inayomkabili ya kunaswa na madawa ya kulevya nchini Afrika Kusini, Video Queen Agnes Gerald ‘Masogange’ amepata balaa jipya, Ijumaa Wikienda lina taarifa kamili.      

 
  Dawa za kulevya.
Kwa mujibu wa chanzo chetu makini ambacho kipo nchini humo, Masogange na mwenzake aliyekamatwa naye, Melisa Edward wamefutiwa dhamana hivyo wamerudi tena rumande.
Agnes Gerald ‘Masogange’.
KWA NINI DHAMANA IFUTWE?
Habari zinadai kuwa, dhamana za wawili hao zimefutwa kufuatia kuhisiwa kwamba wana mpango wa kuondoka nchini huko kinyemela na kurejea Tanzania, jambo ambalo limetafsiriwa kama jaribio la kuikimbia kesi hiyo.
“Unajua huku Sauzi si kila mtu anawaonea huruma Masogange na Melisa kwa tatizo lililowapata, sasa utakuta maskani mtu anaropoka vitu vya ajabu pengine vya uongo bila kujua kuwa si kila mtu anayesikiliza atayaachia hapohapo, wengine ni ‘mainfoma’ wanayafikisha mbele.


“Hicho ndicho kilichomtokea Masogange, wakati baadhi ya watu wakiwa kwenye mchakato wa kumsaidia ili kujua jinsi gani kesi yake itakwenda haraka, wengine wanakwenda kuongea mambo ya ajabu kwa watu wao wanaowatuma kuwapelekea taarifa, eti kuna watu wanajipanga kuwatorosha, si sheria ikafuata mkondo wake.
“Hii inatupa wakati mgumu sisi tuliokuwa tumsaidie, mara kwa mara tunaitwa na kuhojiwa na jeshi la polisi. Ndiyo maana dhamana yao imefungwa, ukiangalia nini kilichosababisha ni maneno ya uongo yanayotokea maskani,” kilisema chanzo hicho ambacho kiliomba hifadhi ya jina lake.

MASOGANGE AKAUKA MITANDAONI
Licha ya kukumbana na kesi ya madawa ya kulevya, Masogange aliendelea kutumbukiza picha zake kwenye mitandao ya kijamii na kuzielezea, lakini baada ya kufutiwa dhamana amekauka mitandaoni kwa picha za karibuni.
“Nyiye si mnaona, siku hizi haposti tena picha zake mpya kama palepale katikati baada ya kukamatwa. Siku zile alikuwa nje kwa dhamana, sasa yupo rumande hawawezi kumwachia akacheza na simu,” kilisema chanzo.

WABONGO WALIOJITOLEA FEDHA KUMWOKOA WASIKITIKA
Baada ya staa huyo kutiwa nguvuni Julai 5, mwaka huu, baadhi ya Watanzania waishio Bongo na kule Afrika Kusini walidaiwa kuchanga fedha kwa lengo la kumsaidia mrembo huyo lakini kufuatia kuvuja kwa taarifa za kufungwa kwa dhamana yake, wamekosa nguvu na kusikitikia kitendo hicho.
Kamanda Nzowa.
SHERIA ZA AFRIKA KUSINI NA TANZANIA KUHUSU ‘UNGA’ SI SAWA?
Inadaiwa kuwa, nchini Afrika Kusini mtu akikamatwa na ‘unga’ anaweza kuwa nje kwa dhamana wakati kesi yake ikiendelea kusikilizwa mahakamani, Tanzania mtu akinaswa na unga kesi inasikilizwa akiwa rumande.

POLISI HAWAKAUKI NYUMBANI KWAKE
Habari kutoka vyanzo vya hapa Bongo zinadai kuwa, askari polisi (kituo cha kazi hakijajulikana) wamekuwa wakifika nyumbani kwa msanii huyo, Kijitonyama, Dar na kuwauliza mambo kadhaa majirani.
“Jamani ishu ya Masogange vipi? Maana hapa mtaani kuna polisi wamekuwa wakija mara kwa mara na kumuulizia kama yupo. Wao hawajitambulishi kama askari lakini watatu kati yao wamebainika ni polisi,” kilisema chanzo hicho.
Kiliendelea kudai kuwa, Julai 20, mwaka huu alifika askari mmoja na kuuliza majirani kama wamewahi kumwona mwanaume mrefu, mweupe akiingia kwenye nyumba ya Masogange.
“Julai 20 alikuja afande mmoja, akawauliza majirani kama kuna siku yoyote ambayo mwanaume mrefu, mweupe aliingia kwa Masogange, akajibiwa hajawahi kufika mtu wa aina hiyo.
“Ndiyo maana nikauliza kesi yake vipi kule Bondeni (Afrika Kusini)? Ila kuna kitu nilikisikia kwa baadhi ya watu kwamba kuna ndugu yake atakuja kuhamisha vyombo vyake kwa sababu wanajua kesi itachukua muda mrefu,” kilisema chanzo.
Masogange.
KUMBUKUMBU
Julai 5, mwaka huu, Masogange na Melisa walinaswa na madawa ya kulevya katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Oliver Tambo mjini Kempton Park, Afrika Kusini.
Ilidaiwa kuwa thamani ya mzigo huo wenye kilo mia moja na hamsini ni shilingi bilioni moja na laki sita.

LULU MICHAEL AMWAGIWA SIFA KWA UZURI WAKE WENYE WIVU MJINYONGE


Producer wa video za muziki Tanzanzia kutoka Arusha, Nisher, leo hii ameamua kumwaga sifa za kutosha kwa muigizaji Elizabeth Michael (Lulu), kupitia mtandao wa Instagram.Nisher amesifia baadhi ya viungo vya mwili vya dada huyo, kama zegembe, miguu, macho pamoja na smile yake.
Kwa mua mfupi tangu alipoingia kwenye utengenezaji wa video, Nisher amefanikiwa kutoa video kali kama "Mama yeyo" ya G Nako feat Ben Pol pamoja na "Jikubali" ya Ben Pol ambayo imefanikiwa kuchezwa kupitia kituo cha Televishen cha South Afrika "Channel o"




HASHEEM THABEET AIBUKIA NDANI YA BONGO STAR SEARCH


Mtanzania pekee anayeiwakilisha Tanzania kwenye ligi ya mpira wa kikapu nchini Marekani maarufu kama NBA, Hasheem Thabeet. Hivi karibuni alijunga na majaji wa Bongo Star Search kwa lengo la kuwapa moyo vijana ambao wanajaribu kuonyesha vipaji vyao kwenye shindano hili. Hasheem Thabeet ni moja ya vijana ambao wamefanikiwa kutumia vema vipaji vyao na kuwa mfano mzuri kwa vijana wengine kufanya juhudi kwenye talent zao.
1014055_583040755079983_1736572220_n
Jaji mkuu wa BSS Rita Paulsen aliandika kupitia ukurasa wake wa facebook kwamba, “Rafiki yangu Hasheem Thabeet alikuja kuwapa moyo na kuonyesha support yake kwa vijana wanaofanya usaili. Namshukuru sana kwa mchango wake”.

ZITTO, MBATIA NA MAKAMBA WATAJWA KWA URAIS 2015


Pia wamo Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii na Dk Hussein Mwinyi na  wa Nishati na Madini Sospeter Muhongo.
Dar es Salaam. Ikiwa imebaki miaka miwili kufanyika ka uchaguzi mkuu nchini, Kamati ya Vijana wapenda Amani Tanzania, imetaja majina ya watu wanne wenye sifa za kuwania urais nchini, huku ikieleza kuwa uzoefu wa miaka mingi si kipimo kizuri cha uongozi bora.
Kamati hiyo imesema Watanzania wanatakiwa kuwaogopa watu wanaojitaja wazi kuutaka urais, huku wakitumia majukwaa ya kisiasa, kidini, kijamii, kiutamaduni na michezo kutoa misaada mbalimbali kwa maelezo kuwa watu hao wakipewa nchi, wataongoza kwa maslahi ya kundi fulani.
Waliotajwa katika orodha hiyo ni Mbunge wa Kigoma Kaskazini na Naibu Katibu Mkuu wa Chadema, Zitto Kabwe, Mwenyekiti wa Chama cha NCCR-Mageuzi, James Mbatia, Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii, Dk Hussein Mwinyi na Naibu Waziri wa Mawasiliano Sayansi na Teknolojia, January Makamba.
Katika orodha hiyo, kamati hiyo haikuwataja viongozi waliowahi kujitangaza kutaka nafasi hiyo na ambao hawajajitangaza, lakini wanaonekana kuwa na dhamira ya kugombea urais mwaka 2015.
Akizungumza na waandishi wa habari jana, Mwenyekiti wa Kamati hiyo Chifu Msopa, alisema wakati umefika kujadili mahitaji ya nchi kiuongozi kwa manufaa ya siku zijazo,.
Katika maelezo yake, Msopa alitaja sifa za kila kiongozi aliyemtaja katika orodha hiyo na kwamba  kama ikitokea watu hao wakashindwa kusimamishwa na vyama vyao kuwania urais mwaka 2015,  kamati hiyo itamuunga mkono  yeyote ambaye atakuwa na sifa zinazofanana na watu hao wanne.
Sifa za waliotajwa
Kwa upande wa ZittoMsopa alisema ana uwezo mkubwa kiungozi, na kwamba mfano ni wa jinsi anavyosimamia Kamati ya Bunge ya Mashirika ya Umma na kufichua madudu.
Kwa upande wa Mbatia, alisema kiongozi huyo ni mzalendo wa nchi yake, ametulia na ana hekima kubwa ya kiuongozi na kwamba busara zake zimedhihirika kwa jinsi anavyoongoza Kituo cha Demokrasia Tanzania (TCD) kama mwenyekiti.
“Amekuwa akipigania ubora wa elimu ya watoto wetu na kujali ujenzi wa taifa bora zaidi na ana uwezo wa kufanya kazi na viongozi kutoka vyama vyote vya siasa.
Akitaja sifa za Makamba alisema wakati akiwa mwenyekiti wa Kamati ya Nishati na Madini alikuwa msema kweli, jasiri kwa kuikosoa Serikali inayoongozwa na chama chake.
Alisema Makamba wakati akiwa Wizara ya Mambo ya Nje, alikuwa msaidizi wa Rais Jakaya Kikwete kwa miaka mitano na kufafanua kuwa hiyo ni sifa ya muhimu kwa kiongozi.
Akimzungumzia Dk Mwinyi, Msopa alisema ana busara na ndio sababu ya kuongoza vizuri wizara nyeti ya Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa.

NANDO WA TANZANIA ALETA UMAREKANI NDANI YA JUMBA LA BIG BROTHER NA KUFUKUZWA NDANI YA JUMBA HILO

Jana usiku mara tu baada ya Sulu na Annabel kutolewa kwa kura za watazamaji, Big Brother aliwaita washiriki pamoja katika kikao cha dharura kufuatia ugomvi uliotokea kati ya Nando na Elikem.

Itakumbukwa kwamba siku ya ijumaa ilitokea hali ya kutoelewana kati ya Nando na Elikem. Wawili hawa walitukanana sana na kutishiana mno. Ugomvi huo ulianzishwa na Nando.

Kwa mujibu wa sheria za Big Brother mwaka huu, kuanzisha ugomvi ni kosa ambalo hupelekea kupata 'strike' ama onyo.

3 strike rule ni mtindo unaotumika msimu huu. Kwa mujibu wa Big brother, yeyote atakaye fanya makosa matatu makubwa na kupewa maonyo matatu basi moja kwa moja anatakiwa atimuliwe..

Sheria hiyo imetumika kumtimua Nando kwa sababu 1. Alianzisha ugomvi siku ya Ijumaa, 2. Alishiriki ugomvi na Elikem na 3. Alitishia maisha, "I feel like stabbing him. A nigga like that deserves to die"...

Katika kipindi cha wiki 9 za ushiriki wake katika jumba hilo, Nando amekutwa na misuko suko kadhaa ikiwemo kuwahi kukutwa na kisu katika Party ya Channel O pia kukutwa na mkasi chini ya kitanda kitu ambacho ni kinyume cha sheria za big brother.

Kutokana na ugomvi huo Elikem alipata strike moja.

Big brother alimtaka Nando aondoke katika jumba lake hilo na kutumia fursa hiyo kuwataka washiriki wengine waishi kama watu wazima.
 
From Big Brother Africa Website
Tanzania's Nando has been disqualified from the Big Brother House.

After tonight's Evictions that saw Annabel and Sulu being given the boot, Big Brother then gathered all of the Housemates in the living room.

Today Big Brother reproached Nando for the fight that he had with Elikem on Friday. The heated face-off with Elikem saw the two fellas exchanging fiery words between them. Nando is the one that instigated the fight. Instigation and provocation is a violation of the Big Brother rules.

For this fight Nando received his second Strike and Elikem was has served with his first Strike. Afterwards the Tanzanian was called into the Diary Room. He was given his third Strike for making threats against Elikem's life, saying: "I feel like stabbing him. A nigga like that deserves to die".

And he was also caught sleeping with scissors under his bed and this is not the first time that he has been caught with a weapon in the House. The troubled young fellow has had a dramatic nine weeks in The Chase. Last month he was served with a a Strike and a stern warning from Big Brother after he was found carrying a knife to the Channel O Party. The possession of weapons or intention to be violent in the House another violation of the Big Brother rules.

After the Diary session Nando was told to immediately exit the House. Big Brother then gave a warning to the Housemates to conduct themselves as adults.

HAUSIBOI ALIYEMLAWITI BINTI WA MIAKA MINNE AHUKUMIWA KIFUNGO CHA MAISHA JELA HUKO MPANDA

 
hausiboyi
Mahakama  ya Hakimu Mkazi ya Wilaya ya Mpanda Mkoa wa Katavi imemhukumu kijana, Baraka  Juma (22) mkazi wa kijiji cha Nkungwi  wilayani humo, kifungo cha maisha jela  baada ya kupatikana  na hatia  ya  kosa la kumlawiti mtoto wa kike mwenye umri  wa  miaka minne  baada  ya kumhadaa na  kumlewesha bia.

Akisoma  hukumu  hiyo  juzi, Hakimu Mkazi Mfawidhi wa Mahakama hiyo, Chiganga Tengwa  alisema ameridhishwa  na  ushahidi  pasipo kutia shaka uliotolewa mahakamani hapo na upande zote  mbili za mashitaka na utetezi.
“Nimelazimika kutoa adhabu  kali  kwa mshtakiwa  baada ya  mahakama  hii kumtia  hatiani  ili  iwe  fundisho  si kwake  tu, lakini  pia  kwa wengine  wenye tabia  kama  yako …. kitendo  ulichomtendea mtoto  huyo  ni  cha kinyama hustahili  kuonewa  huruma, “ alisema Tengwa.
Awali Mwendesha Mashitaka, Mkaguzi wa Polisi, Lazaro Masembo alidai mahakamani hapo kuwa mshitakiwa alitenda kosa hilo Aprili 2 mwaka huu nyumbani kwa wazazi  wa mtoto huyo ambako mtuhumiwa  alikuwa ameajiriwa na wazazi wake kama mfanyakazi wa ndani.
Ilidawa  mahakamani  hapo  kuwa siku hiyo  ya tukio mama mzazi wa mtoto huyo alikuwa amekwenda kijiji cha jirani kutembelea ndugu zake  ambapo  alimwacha mtoto  wake huyo  chini  ya  uangalizi wa mshitakiwa.

Pia  nyumbani hapo  ilidaiwa  mahakamani  hapo  kuwa  kulikuwa  na  msichana  aitwaye Nyasolo Doya (18 ) ambaye  alikuwa  mgeni wa  nyumba hiyo ambaye alifikia hapo  kujifungua.
Kwa mujibu wa Mwendesha Mashtaka, Masembo,  mtuhumiwa alimwita mtoto huyo  sebuleni ambako  alikuwa  amekaa na kisha akaanza  kunywesha  bia aina ya  Balimi  kisha  akamlawiti  huku  mtoto akipiga kelele kwa maumivu akisikika akisema, “mama  nakufa.”
Mahakama  hiyo  ilielezwa  kuwa  kufuatia  kelele za  kilio  cha mtoto  huyo, msichana  Nyasolo Doyo  alishtuka na kulazimika  kukimbilia  sebuleni  ndipo alipomshuhudia  mshitakiwa akimwingilia mtoto  huyo huku akiwa amevua  nguo zake.
Mwendesha Mashtaka Masembo  alisema Nyasolo alipomsihi Baraka amwachie  mtoto  huyo aligeuka ‘mbogo’ na kumtishia  kuwa iwapo atatoa  siri  hiyo kwa wazazi wa mtoto  huyo  atamuua, ndipo  msichana huyo aliponywea kwa hofu  ya tishio  hilo  la  kuuawa.
Mahakama hiyo  ilizidi kufahamishwa kuwa  mama mzazi wa mtoto huyo alirejea nyumbani kwake saa mbili usiku  na ndipo  alipomwona binti yake  huyo akitembea kwa kuchechemea  mwendo  uliomshtua  mama  huyo  na akaamua  kumuuliza msichana Nyasolo  ambaye  alimsimulia mkasa wote  huo wa kusikitisha.
Mwendesha Mashtaka alidai  mahakamani hapo kuwa  mama huyo  alilazimika kumpigia simu baba mdogo wa mtoto huyo ambae anaishi kijiji cha jirani ambae alifika  nyumbani  hapo saa nane usiku na ndipo walipoamua kumfungia mtuhumiwa  mlango wa chumba chake kwa nje na kisha walienda kutoa taarifa kwa uongozi wa kijiji.
Katika shauri hilo upande wa  mashtaka ulikuwa na mashahidi  watano mmojawapo akiwa daktari aliyemfanyia  uchunguzi wa kitabibu mtoto huyo na kuthibitisha  kuwa   alikuwa ameingiliwa na mwanaume katika sehemu zake za siri ambapo  mshitakiwa hakuwa na shahidi yeyote.
Katika utetezi wake, mshitakiwa aliiomba mahakama imwachie huru kwa kile alichokieleza kuwa alisingiziwa tu.