AIBU: MKE AFUMANIWA AKIGAWA URODA CHUMBANI KWA MUMEWE



Timbwili I zito limeibuka baada ya mwanaume aliyetajwa kwa jina moja la Samora kumnasa ‘live’ mkewe Hadija akimsaliti kwa kuvunja amri ya sita  na hawara ndani ya Mwezi Mtukufu wa Ramadhani, tena kwenye chumba chao..

Habari kutoka chanzo cha uhakika kilitonya kuwa Samora na Hadija ni wanandoa waliooana Bomani pale Magomeni, Dar, mwaka 2009 na katika ndoa yao wamebahatika kupata mtoto mmoja wa kiume.

Tukio hilo la fumanizi lilijiri maeneo ya Kinondoni-Kwamsisiri, Dar nyumbani kwa wanandoa hao, majira ya saa 1:00 usiku, Julai 29, mwaka huu.


Habari zilieleza kuwa mwanzoni mwa mwaka huu, ndoa ya wawili hao ilitumbukia nyongo na kuingia kwenye mgogoro ambapo pamoja na kuweka mambo sawa, waliendelea kukwaruzana mara kwa mara.


 Ilidaiwa kuwa chanzo cha wawili hao kuhitilafiana ni kutokana na mwanaume kumtuhumu mkewe kutoa tunda nje ya ndoa.

Ikasemekana kuwa baadaye wapambe walimfuata Samora na kumtonya kuwa mkewe amekuwa na uhusiano wa kimapenzi na kidume mwingine nje ya ndoa yao ndiyo maana amekuwa akimletea nyodo .

  Iliendelea kudaiwa kuwa baada ya ndoa kutibuka, Samora alikuwa mnyonge na mwenye msongo wa mawazo hivyo ikabidi aikimbie nyumba kwa muda na kwenda kwa wazazi wake.

Ilisemekana kuwa, Samora alirejea nyumbani huku akifanya uchunguzi wa nguvu akiwatumia majirani kumpatia taarifa kuhusu kila mwanaume aliyeingia na kutoka nyumbani kwake yeye akiwa hayupo.

 Uchunguzi wa Samora ulibaini kuwa, Hadija alikuwa ‘akibanjuka’ nje ya ndoa na mwanaume aliyetajwa kwa jina moja la Rwekaza ambaye ni mfanyakazi serikalini.


Habari za kina zilisema kuwa, Samora alitonywa kwamba jamaa alikuwa akitimba na gari aina ya Suzuki Swift 1.3 na siku nyingine alikuwa akilala hadi asubuhi bila tone la soni kuwa Hadija ni mke wa mtu.



Baada ya kupata uhakika huo ndipo Samora akajipanga kwa kuwatafuta vijana wa mtaani ili Rwekaza atakapofika nyumbani hapo kulala na mkewe wamvamie na kumfanyizia. 
 

Bila kufahamu kuwa anasubiriwa kwa hamu majira yaa saa 1:00 usiku, Rwekaza huyooo, akatinga nyumbani hapo na moja kwa moja akafikia chumbani kama kawaida yake.

Wakiwa chumbani, ilidaiwa kuwa waliendelea na mambo yao huku Rwekaza akiwa tumbo wazi na suruali yake amefungua zipu huku Hadija akiwa amesaula na kubaki na ‘kufuli’, kisha akajifunga khanga moja.


Katika fumanizi hilo, Samora alitinga chumbani humo akiwa ameambatana na kundi la vijana kibao ambao walikuwa na lengo moja tu, kumfanyia kitu mbaya Rwekaza.
 


Wakiwa chumbani, kuliibuka bonge la timbwili baada ya Samora kumshuhudia mwenza wake aliyekula kiapo cha kutotengana naye akisaliti ‘laivu’ penzi lao.

Baada ya kuona machafuko makubwa ya hali ya hewa chumbani, mwanahabari wetu aliwataarifa polisi katika Kituo cha Kwamsisiri ambao walifika maeneo hayo na kufanya kazi kubwa na nzuri ya kuepusha balaa au mauaji kwa kuwa Samora alikuwa na hasira kali.



Ili kuthibitisha kuwa ni mkewe wa ndoa, Samora alizama kabatini na kuchomoa cheti cha ndoa na picha walizopiga siku ya ndoa yao zikiwaonesha wakiwa na tabasamu la ‘mimi na wewe milele’ kabla ya shetani ‘kufanya yake’ kwenye unganiko lao.


Kwa mujibu wa majirani, tukio hilo liliwasikitisha wengi huku wakiamini kabisa kuwa ni nadra matukio ya mafumanizi kutokea katika kipindi cha mfungo.

“Jamani hata Mwezi Mtukufu? Ni aibu sana kwa mke kuingiza mwanaume mwingine kwenye chumba cha mumewe. Kweli hili fumanizi ni kiboko,” alisikika mmoja wa majirani hao walioshuhudia tukio hilo muda mfupi baada ya kufuturu.
Source: Global publisher

VIDEO:BOW WOW NA TYRA BANKS WANYONYANA DENDA KWENYE TV LIVE

MADUDU UWANJA WA NDEGE DAR ES SALAAM


 
TUKIO la wasichana wawili wa Tanzania waliokamatwa na dawa za kulevya Afrika Kusini, limechukua sura mpya baada ya kujulikana kwamba, siku ambayo watuhumiwa hao walisafiri kupitia Uwanja wa Ndege wa Julius Nyerere Dar es Salaam, mbwa wanaohakiki usalama wa mizigo hawakuwapo. Chanzo chetu cha habari kiliiambia MTAZANIA, kwamba pamoja na uwepo wa kitengo cha kudhibiti dawa za kulevya uwanjani hapo, kitengo hicho kina kasoro kadhaa zinazotakiwa kurekebishwa.
“Mimi niko hapa, najua kila kinachoendelea, nakwambia siku hiyo ambayo wale wasichana walipitisha dawa hizo, hapakuwa na mbwa wa kunusa, naamini kama mbwa wangekuwapo, lazima siri ingefichuka,” kilisema chanzo hicho.
Kwa mujibu wa chanzo hicho, katika viwanja vya ndege kuna vitengo vingi vikiwamo Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), Idara ya Uhamiaji na askari polisi ambapo kila kitengo kina majukumu yake.
“Kwa hiyo, ninachotaka kukwambia ni kwamba, jukumu la Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Tanzania (TAA) ambayo baadhi ya watu wanasema inachangia kupitisha dawa za kulevya, haihusiki kwa sababu jukumu lake kuu ni kuzuia vitu vinavyohatarisha usalama wa ndege na abiria.
“Kuhusu uzito wa mizigo na malipo, hilo linafanywa na shirika la ndege husika na baada ya shughuli zote kufanyika, mizigo hukaguliwa kwa mashine na kunuswa na mbwa kabla ya safari kuanza,” kilisema chanzo hicho.
Pamoja na hayo, utata mwingine juu ya hali ya usalama na uwajibikaji wa watumishi wa uwanja huo wa ndege umejionyesha kupitia nyaraka zilizopatikana.
Uchunguzi uliofanywa na MTANZANIA kwa siku kadhaa sasa, umebaini dawa hizo kilo 150 aina ya Crystal Methamphetamine zenye thamani ya Sh bilioni 6.8 zilizokamatwa na wasichana hao, zilimhusisha pia mshirika wao kibiashara aliyefahamika kwa jina la Mangunga ambaye majina yake matatu tunayo.
Kwa mujibu wa uchunguzi huo, wasichana hao, Agness Gerald (25) na Melisa Edward (24) walisafiri ndege moja na Mangunga wakitoka Dar es Salaam kwenda Afrika Kusini.
Nyaraka hizo zinaonyesha kwamba, wakati Manguga na wasichana hao wakisafiri na ndege ya Shirika la Ndege la Afrika Kusini (SAA), namba SA 189, Julai 5 mwaka huu, walikuwa na mabegi tisa.
Nyaraka hizo zinaonyesha jina la Agness Gerald, kwamba ndiye aliyelipia mabegi hayo, lakini katika sehemu inayotakiwa kuandikwa barua pepe, imeandikwa barua pepe ya Mangunga inayosomeka, Nmangunga@Gmail.com.
Mabegi hayo, yalikuwa na kilo 150 za dawa za kulevya lakini kila mmoja alitakiwa kusafiri na kifurushi cha kilo 20 na hivyo kutakiwa kuwa na kilo 60 wote kwa pamoja.
Baada ya kila mmoja kuwa na kilo 20, zilibaki kilo 90 ambazo walizilipia Dola za Marekani 94 badala ya Dola 450.
Nyaraka zinaendelea kuonyesha kuwa, Mangunga, Agness na Merisa wakati wa safari yao walikaa kiti kimoja kilichokuwa na namba tofauti.
Agness alikaa kiti namba 23B, Mangunga alikaa kiti namba 23D na Melisa alikaa namba 23A.
Naye Mkurugenzi Mkuu wa TAA, Suleiman Suleiman, alipotakiwa kutoa ufafanuzi juu taarifa hizo, alikataa kulizungumzia kwa undani na kusema hana majibu kwa kuwa suala hilo liko katika uchunguzi.
Agness na Melisa, walikamatwa Julai 5 mwaka huu katika Uwanja wa Ndege wa Oliver Thambo nchini Afrika Kusini wakiwa na dawa za kulevya.
Wakati wanakamatwa, walikuwa na mabegi sita kati ya tisa waliyokuwa nayo wakati wanapanda ndege jijini Dar es Salaam.
Inasemekana mabegi matatu yaliondoka na Mangunga ambaye hadi sasa hajulikani alipo.
Source:Mtanzania

NI VITA,MASAA 48 YANAKARIBIA KUISHA,WAASI WA M23 WAAMBIWA WAJISALIMIESHE..VINGINEVYO NI HATARI


U   Wanajeshi wa Brigedi Maalum wakiwa katika mazoezi makali yaliyofanyika hivi karibuni huko Goma Mashariki ya Demokrasia ya congo

 Mmoja wa walinda amani kupitia Brigedi Maalum inayoundwa na wanajeshi kutoka Tanzania, Afrika ya Kusini na Malawi akiwa katika moja ya mazoezi yaliyofanyika hivi karibu huko Goma.
 Kamanda Mkuu wa Misheni ya Kulinda Amani katika Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, ( MONUSCO ) Luteni Jenerali Carlos Albeto dos Santos Cruz ametakanza jana jumanne akiwa Goma kwamba MONUSCO itaanza rasmi kuitumia Brigedi Maalum na ametoa saa 48 kuanzia saa kumi jioni kwa saa za Goma jana siku ya Jumanne waasi wote kusalimisha silaha zao, na kwamba ifikapo saa kumi jioni kwa saa za Goma siku ya Alhamisi Agosti Mosi wale wote ambao watakuwa hawajasalimisha silaha zao watachukuliwa kama tishio la usalama kwa wananchi na MONUSCO italazimika kuwapokonya ikiwa ni pamoja na kutumia nguvu kwa mujibu wa Mamlaka iliyopewa na Sheria zinazowaruhusu kufanya hivyo.
------------------------------

Misheni ya Kutuliza   Amani katika  Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo  ( MONUSCO) imetangaza  kwamba kwa mara ya kwanza itaanza kuitumia Brigedi Maalum ( Force Intervention  Brigade)  katika kudhibiti  eneo  maalum  la usalama  ( security zone ) kuzunguka  mji wa Goma ulioko   Mashariki ya  Jamhuri ya  Kidemokrasia ya Kongo na imewapa  saa 48 waasi kusalimisha silaha zao.

Taarifa iliyotolewa na  MONUSCO na kusambazwa na   Idara ya Mawasiliano ya Umoja wa Mataifa  jana  jumanne,  inaeleza kwamba watu binafsi katika eneo la   Kivu ya Magharibi ambalo linajumisha Goma na  Sake  na ambao hawahusiki na vyombo vya usalama watapewa saa 48 kuanzia saa kumi jana kwa saa za Goma ( Jumanne ) kuzisalimisha silaha zao katika  Misheni hiyo na  kujiunga na mchakato wa DDR/RR unaoratibu upokonyaji, usambaratishaji,  urejeshwaji makwao, kuwaunganisha  na jamii na kuwapatia makazi.  

Baada ya  saa  kumi jioni ya  Alhamisi, Agosti Mosi. Taarifa hiyo inasema. Wale wote ambao watakuwa hawajasalimisha silaha zao watachukuliwa kama  tishio kwa usalama wa  wananchi na MONUSCO itachukua hatua zote muhimu kuwapokonya silaha hizo ikiwa ni pamoja  na kutumia nguvu kama ilivyoainishwa katika Mamlaka na sheria za  ushiriki  za  MONOSCO. 

Kwa mujibu wa taarifa hiyo zaidi ya wananchi milioni moja wanaishi katika eneo dogo la Goma na Sake na kando kando ya barabara  ambayo inawaunganisha na   kambi ya wakimbizi ya Mugungu ambayo ni  makazi ya  muda ya watu  karibu 70, 000 ambao wameyakimbia makazi yao kutokana na mapigano.

Kwa mujibu wa MONUSCO, tangu kati kati ya mwezi Mei eneo hilo limeshuhudia mapigano ya mara kwa mara kutoka kwa kundi la M23 dhidi ya  majeshi ya Serikali  ya  FARDC ikiwa ni  jaribio la   wazi la kutaka  kusonga mbele kuelekea Goma na Sake.

“ Katika mashambulizi hayo, likiwamo la hivi karibuni la Julai 14, M23 walitumia  kiholela silaha zao  za  moto zikiwamo silaha nzito  ambazo zimesababisha  wananchi kujeruhiwa” .
Taarifa hiyo imeongeza kwamba    kundi hilo la M23 katika mashambulizi hayo  limelenga pia Vituo vya Umoja wa Mataifa.
Aidha  taarifa hiyo inabainisha kwamba  eneo hilo maalum la usalama ( security zone)  litasaidia kudhibiti tishio la moja kwa moja  mbali na eneo la  nje ya Goma na pengine  eneo hilo linaweza kupanuliwa na kurudiwa sehemu  nyingine  kutakako hitajika.
 Tamko hilo  la kutoa saa 48 kwa waasi kusalimisha silaha zao  linafuatia kuwasili  katika eneo la Goma kwa  Kamanda Mkuu wa  MONUSCO, Luteni    Jenerali  Carlos Alberto dos Santos Cruz, ambaye alitangaza kwamba  Misheni ya MONUSCO itaunga mkono jeshi la Serikali  ( FARDC)  katika kuanzisha eneo la usalama kuzunguma  eneo la  Goma na vitongoji vyake.
 
Taarifa hiyo inamkariri Kamanda  Mkuu wa MONUSCO akiyapongeza  majeshi ya serikali  kwa  kazi nzuri iliyofanya wiki  iliyopita ya kuwadhibiti M23. Ingawa  anasema eneo la Goma na Sake   bado limo katika mazingira magumu sana na kwamba ni wajibu wa wahusika wote kuhakikisha wahalifu wote hawaendelei kuhatarisha  raia wa eneo hilo.
Kwa mwaka uliopitia , kundi la M23 pamoja na makundi mengine yenye silaha yamekuwa yakipambana mara kwa mara na majeshi ya serikali katika  Mashariki ya Kongo, huku  makundi hayo yenye silaha  mwezi Novemba mwaka jana yakiikalia Goma  kwa muda.
Aidha mapingano ya hivi karibuni  ambayo safari hii yalihusisha pia kundi jingine la wanagambo wenye silaha  lenye asili yake nchini Uganda, yamesababisha zaidi ya wananchi 100,000  kuyakimbia makazi yao na hivyo kuongeza mgogoro  wa kibinadamu katika eneo hilo linalohusisha watu wengine 2.6 milioni ambao wameyakimbia makazi yao huku wengine 6.4 milioni wakihitaji  chakula na  huduma za dharura.
Wakati huo huo,   Kaimu Mkuu wa  MONUSCO  Bw. Moustapha Soumare  katika taarifa  yake ametoa wito kwa pande zote kutafuta suluhu ya kisiasa  kwa   matatizo ya  DRC kupitia Mpango Mpana wa Kisiasa wa Umoja wa Mataifa kuhusu amani, usalama  na  ushirikiano wa maendeleo katika DRC na  eneo la Maziwa  Makuu uliopitisha mwezi wa Februari na viongozi 11 wa Afrika na  Taasisi nne za  Kikanda na Kimataifa.

Aidha akasema  katika  kipindi hiki ambacho suluhu la kisiasa linatafutwa MONUSCO itatumia nguvu iliyonayo kuwalinda wananchi dhidi ya hatari zitokanazo na  makundi ya waasi

Watumia gari kutapeli Sh 470,000/=


POLISI mkoani Dodoma inashikilia watu watatu wakiwemo raia wa nje, kwa tuhuma za kufanya utapeli na kujipatia fedha kwa njia ya udanganyifu katika vituo vya kuuzia mafuta na maduka ya kubadilishia fedha.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Dodoma, David Misime alisema tukio hilo ni la jana katika Kituo cha Camel kilichoko Chuo cha Mipango katika Manispaa ya Dodoma. Misime alisema watu hao walifika katika kituo hicho ambapo kulikuwa na duka na kuagiza soda kisha baadaye kutoa dola 50 ya Marekani.
Inadaiwa muuzaji aliwaambia watu hao kwamba habadilishi fedha, hivyo kuamua kumdanganya kuwa wanahitaji fedha ya Kitanzania kwa ajili ya kwenda kuonesha Misri kama sehemu ya maonesho.
“Wateja hao waliomba wapatiwe noti za 10,000 za zamani ili wao wampatie noti mpya za 10,000 , muuzaji huyo alichambua noti za zamani zipatazo Sh 470,000 na kuwapa kisha wao kumwambia wanazotaka kumbadilishia ziko kwenye gari na kujifanya kwenda katika gari na matokeo yake waliondoka kwa kasi,” alisema Kamanda.
Alisema baada ya watu hao kuondoka kwa kasi, ndipo muuzaji huyo aligundua kwamba ameibiwa na kupiga simu Polisi ambao waliwasiliana na vituo vyote vya mjini na nje ya mji na kufanikiwa kuwakamata matapeli hao katika kituo cha Chanene kilichoko wilayani Chamwino Pori la Mtungutu.
Kwa mujibu wa Kamanda, watu hao walikuwa wakitumia gari aina RAV 4 T. 872 CGE lenye rangi ya damu ya mzee.
Aliwataja watu hao wenye asili ya Kiarabu ni mwanamke Ahlam Hassan, (50) mkazi wa Tanga, raia wa Sudan aliyekuwa dereva Daoud Abdelgawad (39).
Abdelgawad ambaye ni mkazi wa Misri, inadaiwa alikuwa na hati ya kusafiria ikionesha aliingia nchini Julai 19 mwaka huu na viza ya kuishi nchini kwa miezi mitatu.
Wengine wanaotuhumiwa kufanya utapeli huo ni Matata Lawrence (38) ambaye ni dereva na Mkazi wa Gongo la Mboto, Rahma Mahamoud (26) Mkazi wa Dar es Salaam pamoja na Salehe Mnene (40) ambaye ni mkazi wa Manzese, Dar es Salaam. Kamanda wa Polisi amehadharisha wananchi kuwa makini na matapeli.
Aidha ametaka kutoa taarifa haraka polisi juu ya watu wanaowatilia shaka ili hatua za kuwadhibiti zichukuliwe mapema.
chanzo-habari leo

Viongozi watekwa, wamwagiwa upupu


VIONGOZI wa Chama cha Msingi cha Ushirika wa Mazao na Masoko Lenganelo na Diwani wa Mchemo, Mshamu Chituta, wamekamatwa na wanachama, wakafungiwa katika ghala la korosho na kumwagiwa upupu.
Akizungumzia kisa hicho katika Baraza la Madiwani juzi, diwani huyo alisema wanachama hao walishikwa na hasira mkutanoni, baada ya kudanganywa, ndipo walipomkamata yeye na uongozi wa chama hicho na kuwafungia kisha kuwamwagia upupu.
Alitaja wenzake waliopata adhabu hiyo kuwa ni Mwenyekiti wa Chama hicho, Hassan Nakuya, Katibu aliyemkumbuka kwa jina moja la Mnali na msaidizi wake, Ramadhani Mpanga. Chituta alisema uongozi wa chama hicho, ulitangazia wananchi kwenye mkutano huo, kuwa Mkuu wa Wilaya ya Newala, Christopher Magalla, angekuwapo.
Habari kutoka eneo la tukio, zilieleza kuwa viongozi wa chama hicho walitumia jina la Mkuu wa Wilaya kuitisha mkutano wa wanachama, ili kuwavuta wahudhurie kwa wingi. Diwani Mshamu alisema hakuwa anajua kama uongo ulitumika, kwa kuwa siku ya tukio alikuwa na kikao cha Kamati ya Maendeleo ya Kata, lakini aliombwa na Katibu wa Chama cha msingi, asitishe kikao hicho na aende kwenye mkutano wa chama ambao pia ungehudhuriwa na Mkuu wa Wilaya.
Kwa mujibu wa diwani huyo, wanachama waliitika mwito lakini mkutano ulianza bila Mkuu wa Wilaya, wakagundua kudanganywa ndipo wakaamua kuwaadhibu viongozi na yeye kwa kuwafungia ghalani na kuwamwagia upupu.
Alisema walijaribu kuwasiliana na Mkuu wa Wilaya, ili afike kuwanusuru, lakini simu yake haikupatikana hivyo wakakaa ghalani kwa saa kadhaa, mpaka walipomtafuta Mkuu wa Polisi wa Wilaya (OCD), aliyefika kuwafungulia.
Kutokana na malalamiko hayo ya diwani katika Baraza hilo ambalo Magalla pia alihudhuria, Mwenyekiti wa Halmashauri ya Newala, Ashidi Ndembo, alimwomba Mkuu wa Wilaya, kutoa ufafanuzi wa suala hilo, ili kuondoa hali ya sintofahamu baina ya diwani na uongozi wa chama cha msingi. Majibu ya DC Akijibu hoja hizo, Magalla alisema hakuwa na taarifa na mkutano huo na kwamba siku inayotajwa kufanyika mkutano huo, alikuwa kwenye kikao cha Kamati ya Ulinzi na Usalama cha Mkoa mjini Mtwara.
“Nataka nichukue nafasi hii kueleza kwamba sikuwa na taarifa ya mkutano huo, siku hiyo nilikuwa katika kikao mjini Mtwara na simu nilizima kutwa nzima. Nilipoiwasha, nilikuta ujumbe kutoka kwa mtu nisiyemjua, nilipopiga simu nikagundua ni Mwenyekiti wa Chama cha Msingi cha Lenganelo,” alisema Magalla.
Alisema baada ya kumpigia, Mwenyekiti huyo alimfahamisha kuwa alikuwa amefungiwa ghalani na wakulima na alimpigia kutaka msaada lakini simu haikupokewa, ingawa walishafunguliwa. Magalla alionya wanaotumia jina lake kuitisha mikutano ya wananchi kwa kuwa kitendo hicho ni kinyume cha sheria na utovu wa nidhamu, alitaka wahusika wa jambo hilo waache kabla hatua za kisheria hazijachukuliwa dhidi yao.
“Nimesikitishwa sana na kitendo hiki, hasa ninaposikia kinafanywa na viongozi wenzangu. Kwa kweli si jambo jema…tunajua kuna baadhi ya maeneo wananchi wamekuwa hawajitokezi wanapoitwa katika vikao na mikutano, sasa kama viongozi wa eneo hilo wanahitaji msaada wa DC, ni vema wakawasiliana nami na kwa kuwa huo ni wajibu wangu nitakuja,” alisema Magalla.
chanzo-habari leo

MATAPELI WA ONLINE WAAMUA KUTUMIA KISWAHILI KUTAPELI MITANDAONI-ONA HUYU ANAJARIBU KUNITAPELI FACEBOOK


Hii message hapo chini ni mtu amenitumia Facebook anajiita Sandra na picha yake ni hiyo hapo juu , hii ndio ile staili ya kutepeliwa online wanayotumia watu wa West africa..hapo ametumia kiswahili kibovu na inavyoonekani ametumia Google Translate....Angalizo watanzania wenzangu message kama hizi hazina ukweli wowote hao ni Matapeli tu ...Mwisho wa siku utachat nae atakwambia umtumie dola 200 ili kuclear process ili hela zitoke fasta ..ukishatuma anapotea...EMBU CHUKUA TIME KUSOMA HUU UOZO HAPO CHINI...

Pamoja na Upendo na imani
Zangu wapenzi
Habari za leo, matumaini wewe ni faini, ulionipa matumaini na kurudi ujumbe wangu na i pia kama kuona wewe uso kwa uso na i
nadhani wewe ni mtu wa aina i ni kuangalia mbele kwa kutumia mapumziko ya maisha yangu na mimi si kwenda kutoa upendo wangu kwa mtu yeyote, utakuwa kukidhi mimi, hivyo Bila ya kuangalia kwa mtu mwingine.
Mpenzi wangu kuwaambia zaidi juu ya nafsi yangu i ni Miss Sandra Abdul Haleem umri wa miaka 25 kutoka Liberia msichana lakini sasa anaishi hapa nchini Senegal, binti pekee wa Marehemu Dr Abdul Haleem, naibu waziri wa usalama wa Taifa chini ya uongozi wa rais Charles Taylor ambaye sasa ni uhamishoni baada ya wengi nafsi isiyo na hatia waliuawa, baba yangu na mama yangu aliuawa na serikali ya Charles Taylor.
Tafadhali i si kumwambia mtu yeyote isipokuwa wewe na Mchungaji kuhusu kuwepo kwa fedha hii na i kama wewe tafadhali kuitunza siri kwa watu wengine kwa sababu kwa vile ni (PESA) macho yote itakuwa juu yake.
Nakumbuka i imani yenu na kwamba ni kwa nini i ni kutoa habari hii yote!. Upendo wangu ni kwa wewe na wewe peke, i like kusikia sauti yako
tafadhali, piga tu na mimi kwa namba hii (+ 221-772-492-739) Ni yetu Mchungaji simu jina lake ni Mchungaji Baba Paulo Boris na wake anwani ya barua pepe ni (revpaul.boris @ yahoo.com) Kama wewe piga. naye tafadhali kumwambia kuwa unataka kuzungumza na Sandra Abdul Haleem na yeye atampeleka kwa ajili yangu kwa sababu i ni kukaa katika hosteli wanawake.
Mimi tayari habari kuhusu mipango ya benki yangu ya kudai fedha hiyo na kitu tu wao aliniambia ni kuangalia kwa mpenzi wa kigeni ambao kusimama kwa niaba yangu kutokana na hadhi ya ukimbizi wangu.
Utakuwa na 15% ya jumla ya fedha kwa ajili ya kusaidia mimi na fedha iliyobaki itasimamiwa na wewe katika biashara yoyote ya uchaguzi wako wakati i kwenda nyuma ya masomo yangu. Inayohusiana hii i nitakupa baba yangu benki kuwasiliana mara moja na baadhi ya taarifa juu ya kukubalika yako kunisaidia. Marehemu baba yangu ina $ 4,300,000.00 dola za Marekani milioni amana ambayo i ni ya pili ya jamaa. Hivyo wote i haja kutoka kwenu ni vya yako kamili habari ili i unaweza mbele
kwa benki wasiwasi kwa uhamisho.
Mpenzi wangu i nafurahi kwamba Mungu amewaleta kuona mimi nje kutoka hali hii na i ahadi kuwa aina na usawa haja ya wewe katika kila eneo la maisha yangu pamoja na kuwekeza fedha hii tangu i am bado wadogo sana ya kuisimamia.
Kambi hii ni kama gereza na maombi yangu ni kuhamia nje kutoka hapa haraka iwezekanavyo. Mara baada ya benki kuhamisha urithi wangu mfuko wa akaunti yako kisha unaweza kutuma baadhi ya fedha kutoka mfuko kwamba kwa ajili yangu na kuandaa nyaraka yangu kusafiri na kukutana na wewe katika nchi yako. Wapenzi wangu Tafadhali nami kama wewe kuandika mimi nyuma katika hii sanduku yangu ya barua pepe binafsi (sandrahaiem@yahoo.com) ili Kutoka huko mimi itabidi kutuma yangu ya picha nyingine na kukuambia habari zaidi kuhusu mimi kwa sababu ni siri zaidi kuliko kitabu uso.
bye kwa busu nzuri
Ni kusubiri kusikia kutoka kwenu soonest.
Wako milele katika upendo,
Sandra Abdul Haleem

MAAJABU:MWANASHERIA AISHITAKI ISRAEL KWA KIFO CHA YESU



Maajabu mengi sana hugundulika duniani kila siku , lakini kuna kila uwezekano kuwa ajabu lililoko kwenye story hii likawa ajabu la kipekee . Mwanasheria mmoja ambaye ni raia wa Kenya ameibuka na kuzishitaki serikali za Israel na Italia kwa kosa la kuhusika kwenye kifo cha Yesu Kristo .
Mwanasheria huyo Dola Indidis amefungua kesi hiyo kwenye mahakama ya dunia The Hague kule kule ambako rais wa taifa Lake (Kenya ) Mh Uhuru Kenyatta na Makamau wake William Ruto nao wana kesi ya kujibu .
Mwanasheria huyo amesema kuwa lazima serikali za mataifa hayo ziwajibike kwa kitendo cha unyama alichofanyiwa mwanzilishi wa dini ya madhehebu ya Kikristo ambaye ni Yesu aliyesulubiwa msalabani pasipo kuwa na hatia yoyote ya kustahili adhabu hiyo . 
Dola Indidis amefungua shitaka hilo dhidi ya Mfalme wa uliokuwa Ufalme wa Roma Tiberio pamoja na watawala waliokuwa chini yake wakati huo wakiwemo Pontio Pilato na Mfalme Herode pamoja na viongozi wa kiyahudi wakiwemo mafarisayo na masadukayo ambayo kwa pamoja walikula njama ya kumuua Bwana Yesu .

Indidis anasema kuwa ushahidi uko kwenye kitabu kitakatifu Cha Biblia ambayo kila mmoja anafahamu kuwa haisemi uongo . Kwa kuwa wafalme na watawala waliohusika na kitendo hicho hawako hai serikali ambazo mipaka yake ndio ile ile ya iliyokuwa falme ya Roma iliyokuwa madarakani kipindi hicho zitawajibika kwa niaba .
Dola Indidis anasema kuwa vitendo alivyofanyiwa Yesu ni vitendo vya kinyama na ni ukiukwaji mkubwa wa haki za binadamu nay eye kama mwanadamu anahisi kuwa ni jukumu lake kulinda na kutetea heshima ya Yesu Kristo.

Hata hivyo msemaji wa mahakama ya Dunia ambaye hakutajwa utambulisho wake amesema kuwa hakuna kipengele cha kisheria ambacho kinaweza kuruhusu kusikilizwa kwa kesi hiyo kwani ICJ (International Court Of Justice) husikiliza kesi zinazohusu nchi dhidi ya nchi nyingine hivyo kesi hiyo haiwezi hata kufikiriwa . Indidis kwa upande wake bado ana imani kuwa ana kesi ya kuhoji na anaamini kuwa atashinda kesi hiyo.